• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 5:10 PM
‘Nabii Yohana wa Tano’ ahojiwa na maafisa wa DCI, polisi

‘Nabii Yohana wa Tano’ ahojiwa na maafisa wa DCI, polisi

NA JESSE CHENGE

MHUBIRI wa kanisa la Muungano Church for All Nations, Geoffrey Nakalira Wanyama,83, almaarufu ‘Nabii Yohana wa Tano’ ametii agizo la kufika mbele ya maafisa wa Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) na polisi mjini Bungoma kuhojiwa kuhusu kanisa lake.

Inadaiwa kwamba ‘Yohana wa Tano’ aliandika Biblia yake yenye vitabu 93 kikiwemo kitabu cha Agnes, jina ambalo imebainika linafanana na la mmoja wa wake zake.

Kuhojiwa kwake Ijumaa kunajiri baada ya kamanda wa polisi Bungoma Francis Kooli kuzuru nyumbani kwake Jumatatu wiki hii na kumwagiza afike mbele ya maafisa kuhojiwa. Mhubiri huyo amefika mbele ya maafisa hao saa tatu na nusu asubuhi.

Akizungumza na wanahabari ‘Nabii Yohana wa Tano’ amedai Biblia anayotumia yenye vitabu 93 pamoja na amri 12 ni halali kwa sababu “nilikabidhiwa na Mwenyezi Mungu.”

Amesema hakuandika mwenyewe Biblia hiyo jinsi inavyodaiwa na watu.

Amri za tangu jadi zinazofahamika kwa mujibu wa Biblia Takatifu ni 10. Musa alikabidhiwa kwenye kijiwe katika Mlima wa Sinai.

‘Nabii Yohana wa Tano’ amekuwa akihubiri kwa zaidi ya miongo miwili sasa.

Mhubiri huyo anahojiwa siku chache tu baada ya mhubiri mwingine wa kanisa la New Jerusalem Eliud Wekesa almaarufu Yesu wa Tongaren kuchunguzwa na kufikishwa mahakamani. Hata hivyo, Yesu wa Tongaren aliachiliwa baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka.

  • Tags

You can share this post!

Omtatah awasilisha kesi kupinga Mswada wa Fedha 2023

Wetang’ula asuta Azimio

T L