• Nairobi
  • Last Updated October 2nd, 2023 7:00 AM
Omtatah awasilisha kesi kupinga Mswada wa Fedha 2023

Omtatah awasilisha kesi kupinga Mswada wa Fedha 2023

NA RICHARD MUNGUTI

SENETA wa Busia Okiya Omtatah amewasilisha kesi katika Mahakama ya Milimani jijini Nairobi leo Ijumaa akiiomba itie breki Mswada wa Fedha, 2023.

Seneta huyo aliyetofautiana hadharani na Rais William Ruto alipozuru Busia, amesema mswada huo unakiuka Katiba.

Mnamo Jumapili, Mei 28, 2023, Rais Ruto alizuru Busia ambapo seneta huyo alimwambia wazi kwamba Wakenya wanalemewa na gharama ya juu ya maisha.

“Ninasema wewe ni rafiki yangu lakini mbele ya Katiba, katiba ni rafiki yangu mkubwa kuliko wewe. Nimeangalia mswada wako wa fedha na vipengele kama sita vinahitalifiana na Katiba,” seneta Omtatah akamwambia Rais Ruto.

  • Tags

You can share this post!

Upande wa mashtaka waomba Mackenzie aendelee kukaa...

‘Nabii Yohana wa Tano’ ahojiwa na maafisa wa...

T L