• Nairobi
  • Last Updated May 10th, 2024 2:21 PM
Spika apuuza hatua ya EACC kuzima uteuzi wa naibu gavana Nairobi

Spika apuuza hatua ya EACC kuzima uteuzi wa naibu gavana Nairobi

Na COLLINS OMULO

SPIKA wa Bunge la Kaunti ya Nairobi Benson Mutura, amepuuzilia mbali hatua ya Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC), kusimamisha uteuzi wa Bw Paul Mutungi kuwa naibu gavana.

Bw Mutura jana alisema barua ya EACC imepitwa na wakati kwani tayari Bw Mutungi amepigwa msasa na bunge hilo na kuidhinishwa.Alisema tume hiyo ingewasilisha pingamizi zake wakati tangazo kuhusu uteuzi wa Bw Mutungi liliwekwa magazetini na umma ukatakiwa kuwasilisha maoni na pingamizi.

“Isitoshe, vikao vya kumdadisi Mutungi vilifanyika hadharani. Hao EACC walikuwa wapi?” akauliza Spika Mutura.“Awali, tulishirikisha umma na kutangaza nafasi hii, lakini EACC haikusema lolote. Waliibua pingamizi tu na bunge la kaunti lilikuwa limekwisha kumwidhinisha,”akaongeza.

Kupitia barua iliyoandikwa Novemba 29, 2021, asasi hiyo ilisema Bw Mutungi anakabiliwa na kesi ya ufisadi mahakamani. Kulingana na tume hiyo, Bw Mutungi hafai kushikilia wadhifa wa umma.

kulingana na hitaji la sura ya sita ya Katiba.

You can share this post!

Utata kuhusu idadi ya waliofariki Mto Enziu

FAO yaonya kuhusu uvamizi wa nzige

T L