• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 12:18 PM
Waathiriwa wa njaa kupewa pesa

Waathiriwa wa njaa kupewa pesa

CHARLES WASONGA na KNA

SERIKALI kupitia Idara ya kutoa Usaidizi kwa familia zisizojiweza imeanzisha mpango wa kutoa fedha kwa wakazi katika kaunti 23 zilizoathirika na janga la ukame nchini.

Mpango huo maarufu kama “Hunger Safety Net programme” unatarajiwa kuigharimu serikali Sh558 milioni ambapo kila familia athirika itapokea Sh5,400 kila mwezi.

Kuanzishwa kwa mpango huu kutaondoa mpango unaoendelea sasa wa usambazaji wa chakula cha msaada kwa waathiriwa wa baa la njaa katika kaunti hizo.

Katibu wa Wizara anayesimamia idara hiyo, Nelson Marwa alisema, mpango huo wa utoaji wa fedha kwa familia athirika utapunguza gharama ya usambazaji chakula na kuwezesha walengwa kujinunulia chakula.

“Mpango huu wa utoaji fedha pia kwa watu walioathirika na ukame utafaa kwa serikali na familia zilizolengwa,” akaeleza Bw Marwa.

Alisema hayo Jumatano katika eneo la Sajiloni, eneobunge la Kajiado ya Kati, Kajiado baada ya kusambaza magunia 200 ya mchele na magunia 100 ya maharagwe kwa wakazi.

Kufikia sasa, Kaunti ya Kajiado imepokea magunia 3,200 ya mchele na magunia 820 ya maharagwe ambayo yamesambazwa kwa wakazi katika kaunti ndogo zote saba.

Mpango wa usambazaji fedha badala ya chakula cha msaada ulifanyiwa majaribio mnamo Agosti katika kaunti nne za Mandera, Wajir, Marsabit na Isiolo ambapo zaidi ya familia 100,000 zilifaidi.

Wakati huo huo, wanachama wa Kamati ya Bunge kuhusu Kilimo wamegundua sakata ya uporaji wa Sh1.8 bilioni zilizonuiwa kulipwa wakulima wa mahindi.

Wabunge hao pia wanahoji zilikokwenda Sh10.4 bilioni zilizokuwa katika akaunti ya Bodi ya Hifadhi ya Kitaifa ya Chakula (SFR) iliyovunjiliwa mbali mwaka 2020.

You can share this post!

Farasi ni watatu 2022 – Wetang’ula asisitiza

Wijnaldum afungua akaunti ya mabao kambini mwa PSG...

T L