• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 6:55 AM
Wanafunzi wa Eregi ‘waliugua’ hofu ya kufanya mtihani

Wanafunzi wa Eregi ‘waliugua’ hofu ya kufanya mtihani

NA SHABAN MAKOKHA

WANAFUNZI wa Shule ya Upili ya Eregi Girls waliolazwa hospitalini wakiwa na ulemavu wa miguu walikumbwa na wasiwasi wa kufanya mtihani, uchunguzi umethibitisha.

Zaidi ya wanafunzi 108 walilazwa baada ya kuonyesha dalili kama vile kulemaa miguu na mikono, huku wengine wakishindwa kutembea kwa kutetemeka mwili.

Uchunguzi uliofanywa kutoka kwa sampuli zilizochukuliwa kutoka kwa wanafunzi waliokuwa wamelazwa katika Hospitali Kuu ya Kaunti ya Kakamega (KCGH), Mukumu, Iguhu na hospitali za kaunti ndogo ya Shibwe ulionyesha kuwa wanafunzi hao walikuwa na hofu ya kufanya mtihani wao wa mwisho wa muhula.

Afisa Mkuu wa Afya Kaunti ya Kakamega, Dkt Bernard Wesonga alisema wanafunzi hao walipatwa na matatizo ya kisaikolojia.

 

  • Tags

You can share this post!

PENZI LA KIJANJA: Jamaa huoa kwa wakati wake, huwa hapendi...

Babu Owino asuta Ruto kwa maamuzi kupeleka polisi wa Kenya...

T L