• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 5:55 AM
PENZI LA KIJANJA: Jamaa huoa kwa wakati wake, huwa hapendi presha

PENZI LA KIJANJA: Jamaa huoa kwa wakati wake, huwa hapendi presha

NA BENSON MATHEKA

KIPUSA, iwapo umeangukia barobaro ambaye ni chaguo lako la mume, usimharakishe akuoe.

Kwanza unafaa kufahamu siri hii; wanaume huchukua muda kabla ya kuamua kufunga pingu za maisha.

Hivyo basi, haraka yako ni yako, wanaume hawataki presha na ukimsukuma anaweza kubadilisha nia.

Wanaume wengi huwa hawataki vipusa wanaowashinikiza kuwaoa.

“Kumshinikiza mpenzi wako akuoe ikiwa hayuko tayari ni kuharibu wakati. Wanaume hupenda kupatiwa muda wajiandae kikamilifu, wahisi kwamba wako tayari kwa ndoa,” unasema utafiti uliochapishwa katika mtandao wa www.ivillage.com.

Vipusa wanaweza kudhani mwanamume hataki kuwaoa licha ya kuwa kwenye mapenzi kwa muda lakini wataalamu wanasema hakuna mwanaume anayependa kuoa ikiwa hajimudu kifedha.

Bi Susan Huston, mtafiti na mwandishi wa masuala ya kimapenzi, anasema kwamba kila mwanamke huvutiwa na wanaume walio na hulka tofauti ikiwa ni pamoja na uwezo wa kifedha.

“Sisi wanawake tunavutiwa na kutamani mambo tofauti kutoka kwa wachumba wetu. Lakini hakuna mwanamke anayetamani kuolewa na mwanaume asiye na uwezo wa kifedha au asiyekomaa kiakili,” asema Bi Huston.

Hivyo basi, anaongeza, kumpa presha mwanamume kukuoa kabla ya kujimudu kifedha hakutasaidia chochote.

Jambo bora, ni kumueleza kuwa uko tayari kufunga pingu za maisha naye wakati wowote akiwa tayari, hapo utakuwa umeshinda.

Kulingana na Amra Mwangi mwanasaikolojia wa kituo cha Love Care, Nairobi, vidosho wanapaswa kuwaruhusu wachumba wao kujiandaa kikamilifu.

Muhimu ni kuhakikisha ana mipango ya siku za usoni anayekuhusisha kuipanga. Katika kitabu chake Date out of the league, mtafiti wa masuala ya mahusiano ya mapenzi, April Masini, anashauri vipusa kuepuka wasio na mipango ya siku za usoni.

“Ikiwa mchumba wako hakwambii chochote kuhusu maisha ya siku zijazo hasa kuhusu ndoa, basi anakupotezea wakati,” asema.

Watalaamu wa masuala ya mahaba wanashauri vipusa kuwa waangalifu dhidi ya wapenzi ambao wanachukia watu walio katika ndoa. Wanatoa tahadhari kwa kina dada wanaokwamilia katika uhusiano wa kimapenzi hata baada ya wachumba wao kuwaambia kwamba hawako tayari kuoa.

“Haifai kumshawishi au kumshinikiza mwanaume aliyekwambia hayuko tayari kukuoa afanye hivyo,” asema Bi Maina.

Kulingana na utafiti wa www.ivillage.com, wanawake wa kisasa wanasaka wanaume wacheshi wakuwatumbuiza na sio wa kuwaongezea dhiki maishani.

Hivyo basi, usiharibu mambo kwa kumpa presha kwa kuwa haitakuhakikishia furaha katika ndoa.

  • Tags

You can share this post!

Ndung’u azima ndoto ya Mombasa kumegewa sehemu ya mapato...

Wanafunzi wa Eregi ‘waliugua’ hofu ya kufanya...

T L