• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 6:50 AM
Afisa wa polisi aliyeua vijana Eastleigh ana kesi ya kujibu

Afisa wa polisi aliyeua vijana Eastleigh ana kesi ya kujibu

Na RICHARD MUNGUTI

AFISA wa polisi Ahmed Rashid ambaye amepambana kufa kupona asishtakiwe hatimaye amefunguliwa mashtaka ya kuwaua vijana wawili mtaani Eastleigh, Kaunti ya Nairobi.

Rashid alifikishwa mbele ya Jaji Diana Mochache na kukanusha mashtaka mawili.

Rashid alishtakiwa baada ya Jaji Mochache kutupilia mbali ombi kwamba hakuwa na mamlaka ya kuendelea kusikiza kesi hiyo.

Aidha, Jaji Mochache alisema mahakama ina mamlaka ya kusikiza na kuamua kesi hiyo.

Rashid alishtakiwa kuwaua Jamal Mohamed na Dahir Kheri mnamo Machi 31, 2017.

Baada ya kukana mashtaka, Rashid aliachiliwa kwa dhamana ya Sh200, 000.

Jaji Mochache alitupilia mbali ombi la upande wa mashtaka ya kumnyima dhamana.

Mshtakiwa alidaiwa kwamba aliwatwanga risasi Dahir na Mohamed wakiwa wamelala chini.

Mamlaka huru ya kuchunguza vitendo vya uhalifu vya maafisa wa polisi (IPOA), ilimpendekezea mkurugenzi wa mashtaka ya umma (DPP) amshtaki Rashid kwa mauaji.

Jaji Mochache aliamuru kesi hiyo ianze kusikizwa Mei 30, 2023.

  • Tags

You can share this post!

Shakahola: Upasuaji wa maiti kuanza wiki ijayo

Leopards tayari kurarua Bandari Jumapili ugani Kasarani

T L