• Nairobi
  • Last Updated May 6th, 2024 1:13 PM
Shakahola: Upasuaji wa maiti kuanza wiki ijayo

Shakahola: Upasuaji wa maiti kuanza wiki ijayo

NA ALEX KALAMA 

SHUGHULI ya upasuaji wa miili ya waliokuwa waumini wa kanisa la Good News International itaanza wiki ijayo ili kuchunguza na kubaini nini kilichosababisha vifo vyao.

Awali shughuli hiyo ilifaa kuanza leo Alhamisi lakini ikaahirishwa.

Kulingana na mkurugenzi mkuu wa kitengo cha kupeleleza mauaji ya kinyumbani (Homicide Detective) Martin Nyuguto ambaye anaongoza operesheni ya kufukua makaburi ya waliokuwa waumini wa imani potovu katika shamba linalodaiwa kuwa la mhubiri Paul Mackenzie huko Shakahola, Kaunti ya Kilifi ni kwamba shughuli yaupasuaji wa maiti hizo itafanyika katika hospitali kuu ya kaunti ndogo ya Malindi na litafanywa na wapasuaji maiti wa serikali pekee.

Sampuli za vinasaba (DNA) zitachukuliwa na kupelekwa katika maabara ya serekali na kufanyiwa uchunguzi zaidi ili kubaini ukweli kuhusu kilichosababisha vifo vya waumini hao wa dhehebu la Good News International.

Vile vile wale watu ambao wameripoti kupotea kwa jamaa zao watachukuliwa vipimo kisha kufanyiwa ulinganisho na ulinganuo na sampuli za vipimo zilizochukuliwa kutoka kwa maiti hizo ili wale ambao zao zitawiana waweze kupewa miili ya wapendwa wao kwenda kuizika.

  • Tags

You can share this post!

Polisi na raia washiriki michezo kukabiliana na ugaidi na...

Afisa wa polisi aliyeua vijana Eastleigh ana kesi ya kujibu

T L