• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 6:09 PM
Afueni bei ya mahindi ikitarajiwa kushuka msimu wa uvunaji

Afueni bei ya mahindi ikitarajiwa kushuka msimu wa uvunaji

Na BARNABAS BII

NI afueni kwa wakazi wa magharibi ya Kenya kufuatia kushuka kwa bei ya mahindi msimu huu wa kuvunwa kwa zao hilo na kuwasili kwa shehena kadhaa kutoka nchi jirani za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Bei ya maharagwe na maziwa pia imeshuka katika kipindi cha miezi miwili iliyopita baada ya uzalishaji wa bidhaa hizo kuongezeka.

Bei ya mahindi imepungua kutoka Sh6,400 hadi Sh 5,800 kwa gunia kufuatia mavuno ya msimu huu katika eneo la South Rift, Nyanza na sehemu nyingine za magharibi ya Kenya.

Pia, gharama ya mboga imeshuka huku gunia la kabichi ikiuzwa Sh1,300 kutoka Sh 1,800 na Sukumawiki ikiuzwa kwa Sh700 kutoka Sh 1,300 kutokana na kuongezeka kwa uzalishaji wa zao hilo.

Timu ya Wizara ya Kilimo wiki iliyopita ilifanya mkutano na Shirika la Wasagaji Nafaka (UGMA) kuhusu jinsi ya kuharakisha uagizaji wa mazao hayo ili kusaidia kupunguza gharama ya sasa ya unga kutoka Sh230 hadi karibu Sh100 kwa pakiti ya kilo mbili.

“Hapo awali tuliomba kukutana na Mkuu wa Mawaziri, Musalia Mudavadi, ambaye alituelekeza kwa Wizara ya Kilimo kuhusu jinsi ya kutatua bei ya juu ya unga,” alisema Ken Nyaga, mwenyekiti wa UGMA kwa simu.

Alisema mazungumzo hayo yalihusu mbinu kadhaa ambazo zitapunguza gharama ya unga.

“Wanachama wetu wanafaa kuuza mahindi waliyo nayo kwa bei ya sasa wanapojiandaa kushughulikia mahindi kutoka nchi mbili za EAC,” alieleza Bw Nyaga.

Alisema mahindi hayo kutoka Tanzania na Uganda yatasaidia kupunguza gharama ya unga ambayo kwa sasa inauzwa kwa zaidi ya Sh200 kwa pakiti ya kilo mbili.

“Tunatarajia mahindi ya Tanzania yatauzwa Sh5,700 kwa gunia la kilo 90 huku ya Uganda yakiuzwa kwa Sh5,400 na kupunguza gharama ya unga,” alisema Bw Nyaga.

Katibu wa Idara ya Serikali ya ukuzaji wa mimea, Kello Harsama, alisema katika ripoti kwamba waagizaji bidhaa walikuwa na changamoto kupata mahindi meupe kutoka nchi zinazoyakuza katika ukanda wa Afrika Mashariki kutokana na uhaba wa zao hilo.

“Kuna changamoto ambazo zilichelewesha uingizaji wa mahindi ikiwemo uhaba wa zao katika soko la kikanda,” Bw Kello alisema katika ripoti ya awali.

 

  • Tags

You can share this post!

Maandamano: Ni polisi au magenge?

Wanyonyi akung’uta Mandonga ‘Mtu Kazi’

T L