• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 3:16 PM
Afueni kwa waziri wa zamani akiondolewa kesi ya ufisadi wa Sh33 milioni

Afueni kwa waziri wa zamani akiondolewa kesi ya ufisadi wa Sh33 milioni

Na RICHARD MUNGUTI

MKURUGENZI Mkuu wa Mashtaka ya Umma (DPP) Noordin Haji jana alitamatisha kesi ya ufisadi wa Sh33 milioni iliyomkabili aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi Michael Kamau.

Akiwasilisha ombi la kufutilia mbali kesi dhidi ya Bw Kamau, DPP Haji alisema baada ya kutathmini upya ushahidi katika kesi dhidi ya waziri huyo wa zamani “amefikia uamuzi hakuna ushahidi wa kutosha kuthibitisha kesi dhidi ya Kamau na washtakiwa wengine wawili.”

Kuachiliwa kwa Bw Kamau na wahandisi wengine wawilim, Mwangi Maingi na Nicholas Ng’ang’a kumenogesha idadi ya washukiwa wa ufisadi walioachiliwa tangu Rais William Ruto atwae hatamu za uongozi.

Wa kwanza kufaidi na utawala wa Serikali ya Kenya Kwanza ni pamoja na naibu Rais Rigathi Gachagua aliyeshtakiwa kwa ufisadi wa Sh7.3 bilioni.

Mawakili wa Bw Kamau wakiongozwa na wakili Gavana wa Siaya James Orengo hawakupinga ombi hilo.

Hakimu mwandamizi mahakama ya kuamua kesi za ufisadi Victor Wakhumile alitamatisha kesi dhidi ya Bw Kamau chini ya kifungu cha sheria nambari 87(a) cha uhalifu (CPC).

Bw Kamau ambaye ni mwenyekiti wa bodi ya hazina ya kitaifa ya afya (NHIF) alishtakiwa pamoja na Maingi na Ng’ang’a kwa kubadilisha ramani ya barabara ya Kamukuywa-Kapsokwony-Sirisia Kaunti ya Bungoma na kupelekea serikali kupoteza Sh Sh33, 303, 600.

Kamau alishtakiwa 2015 kwa uhalifu huo aliotenda 2007/2008.

  • Tags

You can share this post!

Askofu alalamikia kulazimishwa kubeba kinyesi akiwa seli...

Mke wa Gachagua adai serikali haina uwezo kudhibiti makanisa

T L