• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 5:04 PM
Bei ya kabichi yashuka

Bei ya kabichi yashuka

NA SAMMY KIMATU

BEI ya kabichi imeshuka maradufu katika masoko baada ya mavuno kuwa mengi katika maeneo ambako mboga hiyo hukuzwa.

Katika soko la Muthurwa, Nairobi, bei ya kabichi iliyouzwa kwa kati ya Sh100 hadi Sh130 mnamo Julai 2023 sasa inauzwa kwa kati ya Sh40 na Sh60.

Mwenyekiti wa Soko la Muthurwa, Bw Nelson Githaiga Waithaka. PICHA | SAMMY KIMATU

Mwenyekiti wa wafanyabiashara wa soko la Muthurwa Bw Nelson Githaiga Githinji alisema wateja wana afueni kununua mboga kwa bei rahisi iliyochangiwa na mvua iliyokuwa ikinyesha na manyunyu yaliyosaidia kunawiri kwa mazao mashambani.

“Kabichi ziko kwa wingi sokoni baada ya mvua iliyonyesha na kijibaridi kilichokithiri katika maeneo mengi ambako mboga hiyo hukuzwa. Pia wakulima wamekumbatia mbinu ya unyunyuziaji mimea maji,” Bw Githinji akasema Alhamisi.

Kadhalika, Bw Githaiga amesema bidhaa hiyo hukuzwa kwa wingi katika maeneo ya Mt Elgon, Nandi, Uasin Gishu, Bungoma, Molo, Njoro, Naivasha, Narumoru, Elburgon, Kinagop, Njabini, Meru, Nyeri, Nyahururu, Elgeyo Marakwet, Trans-Nzoia na Murang’a.

  • Tags

You can share this post!

Uchunguzi wazi wa kifo cha Jeff Mwathi waanza

Re-Union FC ina kibarua kupanda ngazi muhula ujao

T L