• Nairobi
  • Last Updated May 5th, 2024 9:50 AM
Uchunguzi wazi wa kifo cha Jeff Mwathi waanza

Uchunguzi wazi wa kifo cha Jeff Mwathi waanza

NA RICHARD MUNGUTI

KIKAO cha uchunguzi wa kubaini kilichosababisha kifo cha mwanafunzi Jeff Mwathi, aliyekuwa akisomea upambaji katika taasisi ya Nairobi Institute of Business Studies (NIBS), kimeanza Alhamisi katika Mahakama ya Milimani, Nairobi.

Akitoa ushahidi wake, mjomba wa Jeff, ambaye aliaga dunia kwenye mazingira tata katika nyumba ya DJ Fatxo, amesema ripoti mbili za upasuaji wa maiti zilionyesha hakukuwa na swala la kutiliwa shaka katika kifo cha kijana huyo.

Lakini mahakama imeambiwa kwamba Jeff hakuwa amevaa chupi wala kujifunga mshipi alipodaiwa kujirusha kutoka kwa orofa ya 10 katika nyumba ya DJ Fatxo mtaani Kasarani, Nairobi, Februari 23, 2023.

Alizikwa nyumbani kwao katika Kaunti ya Nakuru.

Mnamo Juni 8, 2023, wakili Danstan Omari anayewakilisha familia ya mwanafunzi huyo alisema upande wa Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) ulikuwa umeorodhesha mashahidi 35 katika juhudi za kubaini aliyetekeleza mauaji hayo ya kinyama. Mamake kijana huyo, Bi Anne Mwathi akihutubia wanahabari jijini Nairobi wakati huo, alisema anaamini watajua ni nani aliyetekeleza unyama huo na kwamba haki itatendeka.

  • Tags

You can share this post!

Hospitali 260 zafungwa kwa kutokidhi viwango

Bei ya kabichi yashuka

T L