• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 9:50 AM
Familia za watu 48 walioangamia Solai kupokea fidia Sh57.6m

Familia za watu 48 walioangamia Solai kupokea fidia Sh57.6m

NA JOSEPH OPENDA

FAMILIA zilizoathiriwa na mkasa wa bwawa la Solai mnamo Mei 9, 2018, zinatazamiwa kupokea fidia ya jumla ya Sh57.6 milioni baada ya kuafikiana na mmiliki wa bwawa, Bw Perry Mansukh nje ya mahakama.

Bw Mansukh, mmiliki wa bwawa lililopasuka na kusababisha vifo vya watu 48, amekubali kuzifidia familia hizo Sh1.2 milioni kwa kila maisha yaliyokatizwa ya mtu mzima na Sh800,000 kwa kila mtoto aliyefariki.

Mazungumzo yaliyofanyika Jumanne, Taifa Leo imebaini, yalihusisha wawakilishi kutoka familia 48, Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP), mawakili wa wamiliki wa mabwawa, na wamiliki wenyewe.

Wakili Boniface Masinde anayewakilisha mmiliki wa bwawa hilo, alithibitisha kwamba pande zote zilikutana Solai ili kukamilisha na kuafikiana huhusu mpango huo kufuatia mazungumzo.

Bw Masinde alisema kuwa mahakama iliruhusu pande zote kujaribu kusuluhisha kesi hiyo nje ya mahakama.

Kesi iliwasilishwa na waathiriwa.

Vile vile, Tume ya Haki za Kibinadamu Nchini Kenya, inayowakilisha familia 29, ilithibitisha mpango huo kupitia kwa meneja wao wa mipango Bi Mary Kambo.

  • Tags

You can share this post!

Amerika kwa mara nyingine yapatanisha Rwanda na DRC

FASIHI SIMULIZI: Soma kisa kifuatacho kisha ujibu maswali

T L