• Nairobi
  • Last Updated February 26th, 2024 8:50 AM
Amerika kwa mara nyingine yapatanisha Rwanda na DRC

Amerika kwa mara nyingine yapatanisha Rwanda na DRC

Na MASHIRIKA

KIGALI, RWANDA

AMERIKA kwa mara nyingine imejaribu kuleta upatanisho kati ya marais wa Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kwa lengo la kupunguza uhasama kati ya nchi hizo jirani.

Waziri wa Masuala ya Kigeni wa Amerika Antony Blinken alizungumza na Rais wa Rwanda Paul Kagame na mwenzake wa DRC Felix Tshisekedi mnamo Jumanne jioni, kulingana na taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari na msemaji wa Wizara hiyo Mattthew Miller.

“Kwenye mazungumzo yake na marais hao wawili, Waziri alijadili hali hiyo ya uhamasa na hali mbaya ya kibinadamu inayoshuhudiwa karibu na mpaka wa Rwanda na DRC. Waziri huyo alihimiza kwamba uhasama huo umalizwe kwa njia ya kidiplomasia na kila nchi iondoe wanajeshi wake katika maeneo ya mpaka,” akasema Miller.

Baada ya mazungumzo kati ya Blinken na Kagame, kwa njia ya simu, Ikulu ya Rwanda ilisema inaunga mkono haja ya “kupunguza uhasama na kukumbatiwa kwa suluhu ya kisiasa kwa mapigano nchini DRC.”

Ilisema Rais Kagame anaunga mkono juhudi za sasa za kuleta amani DRC zinazoendeshwa na mataifa ya ukanda wa Afrika Mashariki.

Kuna michakato miwili inayolenga kupata suluhu kwa mzozo unaoshuhudiwa mashariki mwa DRC.

Mchakato unaosimamiwa na Kenya unaendeshwa chini ya mwavuli wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kwa lengo la kukomesha vita kati ya mamia ya makundi ya wapiganaji yanayojulikana kama “mai mai” na kundi kubwa la waasi wa M23.

Aidha, kuna mchakato unaosimamiwa na Angola na unaolenga kukomesha uhasama kati ya Rwanda na DRC.

Ukosefu wa amani mashariki mwa DRC, haswa mkoa wa Kivu Kaskazini, unaweza kuathiri uendeshwaji wa uchaguzi mkuu ulioratibiwa kufanyika Desemba 20, 2023.

  • Tags

You can share this post!

Mfanyakazi wa kaunti akiri mashtaka ya ufisadi

Familia za watu 48 walioangamia Solai kupokea fidia Sh57.6m

T L