• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 8:55 PM
FASIHI SIMULIZI: Soma kisa kifuatacho kisha ujibu maswali

FASIHI SIMULIZI: Soma kisa kifuatacho kisha ujibu maswali

HAPO zamani za kale paliishi mtoto katika bustani fulani. Siku moja, alipokuwa akitembea katika bustani hiyo aliona ua lililokuwa liking’aa na kumeremeta. Mtoto huyu alishangaa lilikotoka ua hilo licha ya kuwa hakuna mtu aliyekuwa amelipanda. Aliita watoto wenzake ili aende kuwaonyesha ua hilo.
Walipolikaribia, lile ua lilianza kugeuka na kuchukua sura ya binadamu. Walijaribu kulishika ila likatoa mngurumo kama simba. Watoto hawa waliogopa na kushikwa na wasiwasi mithili ya kuku mgeni. Walitoroka na kujificha katika chaka lililokuwa mkabala wa bustani. Mmoja wao alichukua jiwe na kuligonga. Ghafla bin vu, ua liligeuka na kubadilika kuwa jitu kubwa la ajabu. Liliwakimbiza na kuwashika kwa mikono mipana na mirefu. Liliwameza wote kisha likalala fofofo kwa shibe.
Karibu na eneo hili, kulikuwa na mtu aliyekuwa akilisha mifugo wake huku akipalilia shamba la mikahawa. Alipoona hivyo alikimbia mwendo wa chui na kulidunga dude hilo tumboni kwa kiserema chake. Punde tu watoto walichomoka kutoka tumboni wakiwa hai na buheri wa afya. Jitu lilikata kamba kisha wanakijiji wakasherehekea maajabu haya.

(a) Bainisha kipera hiki.

Ngano ya mazimwi kwani kuna matumizi mengi ya fantasia na kisa kinahusisha jitu.

(b) Eleza mambo yanayoonyesha kipera hiki ni sanaa.

Mandhari yamesawiriwa kwa ufundi mkubwa.
Wahusika wamejengwa kwa ufundi.
Lugha imetumika kwa ufundi na upekee mkubwa.

(c)Unakusudia kutumia mbinu ya mahojiano kutafiti kuhusu utungo huu. Eleza manufaa manne.

Ninaweza kung’amua wakati mhojiwa anatoa habari zisizo za kweli.
Nitafafanulia mhojiwa maswali ili kuweza kupata habari sahihi zaidi.
Nitapata sifa za uwasilishaji kama vile toni/kiimbo.
Nitapata habari za kutegewa na kuaminika zaidi.

(d)Bainisha shughuli ya kiuchumi zinazoendelezwa katika jamii hii.

Kilimo – Akipalilia shamba.
Ufugaji – Akilisha mifugo.

 

-Na Julian Kihara, Kianda School

  • Tags

You can share this post!

Familia za watu 48 walioangamia Solai kupokea fidia Sh57.6m

Polisi wagundua waliyemsaidia kupata matibabu ni jambazi...

T L