• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 8:50 AM
Itumbi aomba mahakama kuu isitishe kesi ya vitisho dhidi ya DP Ruto

Itumbi aomba mahakama kuu isitishe kesi ya vitisho dhidi ya DP Ruto

Na RICHARD MUNGUTI

MWANAHARAKATI wa Chama cha Kisiasa cha United Democratic Alliance (UDA) Dennis Itumbi amepinga katika mahakama kuu kesi anayoshtakiwa kughushi barua iliyodai kulikuwa na njama za kumuua Naibu wa Rais Dkt William Samoei Ruto.

Anaomba mahakama ifutilie mbali kesi hiyo akisema haki zake zilikandamizwa. Bw Itumbi aliyefika kortini kwa mara ya kwanza tangu atekwe nyara na kujeruhiwa alikuwa akitembea kwa mikongojo. Bw Itumbi aliomba hakimu mkuu Bi Martha Mutuku asitishe kusikizwa kwa kesi inayomkabili kusubiri uamuzi wa mahakama kuu.

Katika kesi aliyowasilisha mahakama kuu Bw Itumbi amedai polisi walikiuka haki zake kumfungulia shtaka la kughushi barua aliyosema iliandikiwa katika Cyber kisha ikadaiwa ni yeye (itumbi) aliyoiandika. Wakili Majimbo Georgiadis anayemwakilisha Bw Itumbi alieleza korti ushahidi unaosubiriwa mahakama kuu ni ule uliowasilishwa mbele ya Bi Mutuku.

“Tunasubiri nakala za ushahidi uliowasilishwa mbele ya Bi Mutuku ndipo mahakama kuu itoe maagizo,” Bw Majimbo alisema. Kiongozi wa mashtaka Bi Alice Mathangani alisema ushahidi huo unaendelea kupigwa chapa na ukikamilika mshtakiwa atapewa.

Bw Itumbi anayeshtakiwa pamoja na mwanaharakati Samwel Gateri Wanjiru kwamba mnamo Septemba 2021 walipatikana wako na kesi ya kijibu kwa kughushi na kusambaza katika mitandao ya kijamii kulikuwa na njama za kumuua Dkt Ruto.

Kesi hiyo itatajwa Machi 10,2022.

You can share this post!

Rao ajitetea dhidi ya madai ya ufisadi katika kiwanda cha...

ICC: Shahidi apandwa na hasira akidaiwa si mwaminifu

T L