• Nairobi
  • Last Updated May 20th, 2024 9:16 PM
Kaunti zatenga pesa chache za bima ya afya

Kaunti zatenga pesa chache za bima ya afya

NA DANIEL OGETTA

SUALA la kaunti zenye idadi ya chini ya wakazi waliosajiliwa katika mipango ya bima ya afya, kutenga mgao mdogo sana kwa ajili ya idara za afya kwenye bajeti ya 2023/2024, limeibua wasiwasi miongoni mwa Wakenya.

Hulka hii imeshuhudiwa katika kaunti za Tana River ya gavana Godhana Dhadho, Mandera ya Mohamed Adan, Garissa ya Nathif Adan, West Pokot ya Simon kachapin na Marsabit ya Mohamud Mohammed Ali, ambako kati ya wakazi tisa kati ya wakazi 10 hawajui lolote kuhusu bima ya afya.

Isitoshe wakazi wa kaunti hizo hawajasajiliwa katika mpango wowote wa bima ya afya, na afya ya jamii zao ndio inatengewa mgao wa chini katika pesa za matumizi ya nyumba zao.

Kulingana na ripoti ya hali ya afya nchini iliyotolewa mwezi jana, chini ya asilimia nane ya nyumba katika kaunti hizo hazijasajiliwa katika mpango wa kitaifa wa bima ya afya (NHIF) au kuwa na bima nyingine yoyote.

Kulingana na bajeti ya kaunti hizo ya mwaka 2023/2024, fedha zilizotengewa idara ya afya inawasilisha mapato yanayotokana na idara ya afya za kaunti hizo.

Kwa mfano kaunti ya Mandera, idara ya afya imetengewa Sh 2.1 bilioni licha ya kupata Sh 11.6 bilioni kutoka kwa serikali kuu.

Kwa upande mwingine, kaunti zilizowekeza katika afya ipasavyo kama vile Laikipia, Nairobi na Nyeri zina idadi kubwa ya watu waliosajiliwa katika mpango wa bima ya afya ya NHIF au zile za kibinafsi.

Serikali hizo pia zinavuna kiwango kizuri cha fedha kutokana na kuwekeza huko.

Hali ya kaunti zisizo na ufahamu wa bima ya afya inadhihirika katika kaunti ya Tana River, ambako asilimia 94.7 ya wakazi hawafahamu lolote kuhusiana na bima ya afya.

Hii ni licha serikali ya kaunti kutojali, wakazi hao na hali waliyomo.

Serikali ilikuwa imefanya mabadiliko katika tozo za bima ya NHIF.

Licha ya hayo, watu saba au zaidi hawafahamu lolote kuhusu bima ya afya kati ya angalau kaunti 34, suala linalodhihirisha umuhimu wa kuwekeza kazidi katika afya.

Taarifa zinaeleza kuwa Mkenya wa kawaida huenda akajipata akiwa masikini endapo atakumbwa na ugonjwa mmoja, ambao utahitaji fedha nyingi za matibabu.

Haya yakijiri, magavana kadhaa wamekosa uvumbuzi wa jinsi ya kuwekeza ipaswavyo katika sekta ya afya, jambo linalohatairisha maisha ya Wakenya.

Kulingana na sheria ya mgao wa fedha ya kaunti ya 2023, kaunti ya Nairobi iliongoza kaunti zingine kwa kutenga sehemu kubwa ya mgao wa Sh 20 bilioni katika sekta hiyo.

Kaunti ya Lamu ambayo mgao wake haukuwa mkubwa sana Sh 3.2 bilioni ilitenga zaidi ya thuluthi moja ya mgao huo kwa ajili ya afya.

Hii ni licha ya angalau wakazi watatu kwa 10 kufahamu kuhusu mipango ya bima ya afya.

 

 

  • Tags

You can share this post!

Ashangaza kutoa kilemba akiteta Mungu ‘amemuacha’ baada...

Raila atishia kufufua maandamano ampa Ruto siku 30

T L