• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 10:50 AM
Kindiki: Wenye mabaa na vilabu kuomba upya leseni

Kindiki: Wenye mabaa na vilabu kuomba upya leseni

NA SAMMY WAWERU

SERIKALI imetangaza kuwa wenye mabaa na vilabu wataomba upya leseni ili kuruhusiwa kuhudumu.

Waziri wa Usalama wa Ndani na Mikakati ya Serikali, Prof Kithure Kindiki alisema Jumatatu, Juni 12, 2023 kwamba hatua hiyo itasaidia katika oparesheni kukabiliana na kero ya pombe haramu nchini.

Akitoa tangazo hilo akiwa katika ziara Meru, Waziri alisikitikia kampeni za awali kuzima pombe haramu kugonga mwamba kwa sababu ya mtandao wa makateli.

“Vita dhidi ya pombe haramu ilianza kitambo na kwa sababu ya makateli walioteka nyara sekta ya pombe, ikawa vigumu kuzima vileo hatari na vyenye sumu,” Prof Kindiki alisema.

Alitaja mtandao wa pombe kama uliosheheni mawakala wenye ushawishi mkuu, na hutumia mamlaka yao kuhonga viongozi wa kisiasa kuwalinda.

Waziri alisema kwa sababu ya kukithiri kwa ufisadi, vita dhidi ya pombe haramu imekuwa kibarua kuangazia.

“Makateli katika sekta ya pombe wamekita mizizi, na katika serikali za awali walilindwa na viongozi wa kisiasa.”

Prof Kindiki alitoa tangazo la uombaji upya leseni kwa wahudumu wa mabaa na vilabu, katika hafla iliyohudhuriwa na Naibu Rais Rigathi Gachagua Kaunti ya Meru.

Bw Gachagua ameapa kuangamiza kero ya pombe haramu nchini, akisema “nuko tayari kuenda nyumbani ikiwa vita dhidi ya vileo hatari na dawa za kulevya ndivyo vitaniondoa mamlakani”.

Oparesheni kali inaendelezwa eneo la Mlima Kenya na Bonde la Ufa, Gachagua akiahidi maeneo mengine ya nchi yatafuata nyayo hizo.

  • Tags

You can share this post!

Wakazi walaumu MCA kwa unyakuzi wa ardhi

Joseph Yobo aamini Kenya ina wanasoka wenye uwezo wa...

aaronmalcolm48