• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 11:55 AM
Kunipigia kura haikumaanisha mkatalie na Hasla Fund, mrudishe hiyo mikopo, Ruto aambia Wakenya

Kunipigia kura haikumaanisha mkatalie na Hasla Fund, mrudishe hiyo mikopo, Ruto aambia Wakenya

NA GEORGE MUNENE

RAIS William Ruto ametaka Wakenya kulipa mikopo ya Hasla Fund waliyochukua kuanzisha biashara zao.

Akizungumza katika Kaunti ya Embu Ijumaa, Dkt Ruto aliapa kuhakikisha waliochukua mikopo hiyo ambayo inatozwa riba ya asilimia nane inalipwa yote.

“Hasla Fund si pesa za bure. Huo ni mkopo na ni pesa ambazo lazima zirudishwe kwa serikali,” akasema.

Aliwakumbusha Wakenya kwamba mikopo hiyo ilitolewa kuwasaidia kuanzisha biashara na kuimarisha maisha yao.

“Tulitaka Wakenya kufaulu kujipatia mkopo kwa njia rahisi kujinufaisha kibiashara na hawafai kuichukulia kama kwamba ni pesa za bwerere. Kuna watu wanasema walinipigia kura na hivyo wanastahili kubaki na pesa hizo, la, si hivyo, haikubaliki. Pesa zilizotolewa ni deni na lazima zilipwe,” akasema.

Aliahidi kuzindua mkondo wa pili wa hazina hiyo wakati wa sikukuu ya Madaraka Dei ili Wakenya wanufaike zaidi.

“Katika Mkondo wa Pili, Wakenya watafaulu kujipatia kati ya Sh20,000 na 200,000 za mkopo huu bila mdhamini yeyote.”

Alitaka Wakenya kuendelea kujikuza kibiashara kwa kutumia fedha hizi.

Kiongozi wa Taifa alikuwa ameandamana na naibu wake, Rigathi Gachagua katika ziara hiyo Embu ambapo pia alipigia debe mpango wake wa kutoza ushuru wa nyumba wa asilimia 3 kwa kila mtu anayepokea mshahara nchini ili kujenga nyumba ‘nafuu’.

  • Tags

You can share this post!

Kamati teule yaambiwa Mackenzie alitumia genge kuua wafuasi...

Maafisa wang’oa na kuteketeza bangi iliyopandwa kando...

T L