• Nairobi
  • Last Updated May 14th, 2024 7:55 AM
Kuria akaangwa kwa kutaka ushuru wa mitumba upandishwe hadi aslimia 25

Kuria akaangwa kwa kutaka ushuru wa mitumba upandishwe hadi aslimia 25

NA CHARLES WASONGA

KWA mara nyingine wafanyabiashara na Wakenya wanaotegemea biashara za nguo zilizotumika, maarufu kama mitumba, wamemsuta Waziri wa Biashara Moses Kuria kwa kupendekeza nyongeza ya ushuru kwa nguo hizo zinazoagizwa kutoka ng’ambo.

Wakiongozwa na mwenyekiti wa Chama cha Wauza Nguo za Mitumba Nchini (MCAK) Teresia Wairimu wanasema hatua hiyo itawaathiri zaidi wakati huu ambapo gharama ya maisha ingali juu.

“Sisi kama mahasla tumemuomba Bw Kuria na serikali hii ya Kenya Kwanza ikome kutunyonga zaidi kwa kuongeza ushuru wa mitumba kwa sababu tayari tupanda kwa gharama ya maisha. Isitoshe, bei ya nguo hizi imepanda kutokana na kudorora kwa thamani ya Shilingi ya Kenya dhidi ya sarafu za kigeni,” anasema.

Akiongea Jumatatu, Agosti 14 katika mkutano wa wadau katika sekta ya utengenezaji nguo mjini Eldoret Bw Kuria alisema serikali itaweka ushuru wa kima cha asilimia 25 kwa nguo zinazoingizwa nchini kutoka, zikiwemo mitumba.

“Hatua hii itasaidia kufufua viwanda vya humu nchini vya kutengeneza nguo ambavyo vimefifishwa na kunawiri kwa biashara ya nguo za mitumba zinazougwa kwa bei nafuu,” Bw Kuria akasema.

Wakenya kwenye mitandao ya kijamii nao wamemrukia Waziri Kuria kwa kumtaja kama nduma kuwili asiyethamini masilahi ya Wakenya masikini.

“Wakati wa kampeni Kuria na wenzake katika Kenya Kwanza ndio walikuwa mstari wa mbele kumshutumu Raila alipopendekeza kupiga marufuku mitumba. Sasa mbona wao wanataka kuongeza ushuru wa mitumba na kuzifanya kuwa ghali? Si hii ni sawa na kupiga marufuku nguo hizi tunazozitegemea kujikwatua?” anasema Abraham Bore.

  • Tags

You can share this post!

Ajivunia kuwa askari wa kaunti baada ya kiwango cha elimu...

KINAYA: Wenye hisa za Kenya wakate miti tusijinyonge!

T L