• Nairobi
  • Last Updated May 1st, 2024 7:02 PM
Lilian Mbogo aondolewa lawama ya uporaji mamilioni NYS

Lilian Mbogo aondolewa lawama ya uporaji mamilioni NYS

NA RICHARD MUNGUTI

ALIYEKUWA Katibu wa Vijana Lilian Mbogo Omollo ameachiliwa huru katika kesi ya kashfa  ya mamilioni ya pesa ya shirika la Huduma ya vijana kwa taifa (NYS).

Bi Omollo aliachiliwa na hakimu mkuu mahakama ya Milimani Nairobi Lucas Onyina aliyeelezwa na Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) hakuhusika na kashfa hiyo.

Bi Omollo alishtakiwa kuidhinisha malipo ya mamilioni ya pesa kwa kampuni za watu wa familia moja.

Ofisi ya DPP ilieleza Onyina kwamba wakati wizi wa pesa za NYS ulitendeka, Omollo hakuwa ameteuliwa Katibu Mkuu Wizara ya Ugatuzi na Masuala ya Vijana.

Miongoni mwa walioshtakiwa pamoja na Omollo ni pamoja na aliyekuwa mkurugenzi mkuu wa NYS Richard Ndubai.

Washukiwa hawa walikabiliwa na mashtaka 82 ya matumizi mabaya ya mamlaka na uporaji wa pesa za umma.

Wakurugenzi wa kampuni nne zinazomilikiwa na watu wa familia moja ya Naivasha walishtakiwa pamoja na Bi Omollo, Ndubai na wengine.

Bi Anne Wambere Ngirita alidaiwa alilipwa zaidi ya Sh50 milioni pasi kutoa huduma zozote kwa NYS.

Anne na dada zake, ndugu yake na mama yao ni miongoni mwa walioshtakiwa katika kashfa hii ambayo viongozi wa mashtaka waliambia mahakama katika taarifa ya utangulizi kuwa Sh8 bilioni zilitoweka katika kashfa hiyo.

Pia kutoandaa ipasavyo ushahidi katika kesi hiyo ya Sh226 milioni kulifanya mahakama inayoisikiliza kulia hoi.

Baada ya uzembe wa DPP na DCI wa kutowapa washukiwa ushahidi kujianika hadharani, ilibidi Bw Ogoti atoe maagizo mapya kwamba washtakiwa wote wapewe ushahidi.

Ushahidi uliosababisha tumbojoto ulikuwa wa malipo ya Sh19 milioni na Sh5 milioni mtawalia kwa kampuni za Njewanga Enterprises na Ngiwaco Enterprises.

Kampuni hizi zinamilikiwa na Phyilis Njeria Ngirita na Lucy Wambui Ngirita.

Kampuni za familia hii ya Ngirita imedaiwa zilipokea mamilioni ya pesa kutoka NYS bila kutoa huduma.

Walioshtakiwa ni Anne Wambere Ngirita, Lucy Wambui Ngirita, Phyilis Njeri Ngirita na ndugu yao Jeremiah Gichini Ngirita.

Aliyekuwa katibu mkuu wizara ya ugatuzi Bi Lillian Omollo alishtakiwa kuidhinisha malipo ya Sh54.8 milioni kwa Anne, Sh63.2 milioni kwa Lucy, Sh50.9 milioni kwa Phyilis na Sh57.8 milioni kwa Jeremiah kinyume cha sheria.

  • Tags

You can share this post!

Maiti bila kichwa na mikono yapatikana katika shamba la...

Tatizo la wanawake kunenepa kupita kiasi lazidi –...

T L