• Nairobi
  • Last Updated May 24th, 2024 2:08 PM
Maandamano kufanywa nje ya makazi ya Uhuru

Maandamano kufanywa nje ya makazi ya Uhuru

Na MWANGI MUIRURI

WANDANI wa Rais William Ruto katika eneo la Mlima Kenya wakiongozwa na Naibu Rais Rigathi Gachagua wamefichua mipango ya kufanya maandamano nje ya makazi ya Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta mjini Kiambu.

Hii inalenga kulalamikia vitendo vya Bw Kenyatta hivi majuzi vya kujitosa kwenye ulingo wa siasa ambapo anapigania kudhibiti Chama cha Jubilee.

Viongozi hao wameapa kuungana pamoja kupinga ushawishi wa Bw Kenyatta katika siasa za humu nchini hadi atakapokubali kuwa uongozi eneo hilo haumtegemei tena.

“Huenda ikawa hivi karibuni kama wiki ijayo. Tutaandaa mkutano huo si kwingine bali nje ya makazi ya familia ya Kenyatta katika kijiji cha Ichaweri, Gatundu Kusini,” alisema Waziri wa Biashara Moses Kuria.

Akizungumza katika Uwanja wa Thika mnamo Jumapili katika hafla ya 25 ya mwimbaji Muigai wa Njoroge, Waziri Kuria alisema,” ni sharti tumpe funzo Uhuru kwamba hata sisi tulizaliwa namna alivyozaliwa na ni lazima azoee kuwa sisi ndio tupo mamlakani.”

Bw Gachagua aliyekuwa mgeni wa heshima alimpa Bw Mr Muigai zawadi yake binafsi pamoja na ya Rais kiasi cha jumla ya Sh2 milioni.

  • Tags

You can share this post!

Sakaja kutimua wafanyakazi 715 waliokuwa wameajiriwa na NMS

TAHARIRI: Uchunguzi wa Shakahola usivurugwe kivyovyote

T L