• Nairobi
  • Last Updated May 1st, 2024 7:02 PM
Maanzo, Otiende Amollo kuongeza ladha kesi ya kupinga Sheria ya Fedha

Maanzo, Otiende Amollo kuongeza ladha kesi ya kupinga Sheria ya Fedha

NA RICHARD MUNGUTI

MALUMBANO makali yanatarajiwa katika Mahakama Kuu kwenye kesi ya kusitisha Sheria ya Fedha ya 2023 ambapo serikali imepigwa breki kuwatoza wananchi ushuru.

Seneta wa Busia Okiya Omtatah ameanza kutifua kivumbi kwa kuomba Spika wa Bunge la Seneti Amason Kingi ashurutishwe kufika kortini kujibu maswali sababu ya kutoshirikishwa kwa bunge hilo katika mjadala wa Mswada wa Fedha.

Bw Omtatah amesema Kingi alikiuka sheria alipokataa kudai Spika wa Bunge la Kitaifa Moses Wetang’ula awasilishe mswada huo wa Fedha katika Bunge la Seneti kujadiliwa kabla ya kupelekewa Rais William Ruto kuutia saini ndipo uwe sheria inayowezesha wananchi kutozwa kodi.

Akiomba Jaji Mugure Thande amwamuru Kingi afike kortini kuhojiwa, Bw Omtatah amesema Spika wa Bunge la Seneti alitelekeza majukumu yake alipomwandikia barua Bw Wetang’ula na kumweleza suala la sheria ya fedha haihusu serikali za kaunti.

“Naomba hii mahakama iamuru Kingi afike kortini kuhojiwa kwa sababu ya msimamo wake kuhusu Sheria ya Fedha 2023,” akasema Omtatah katika ombi lake.

Bw Omtatah amesema Bunge la Seneti halikuhusishwa kwa mujibu wa sheria katika Mswada wa Fedha kabla ya kupitishwa kuwa Sheria ya Fedha, 2023.

Jaji Thande alisitisha kutekelezwa kwa sheria hiyo hadi kesi aliyoshtaki Omtatah isikilizwe na kuamuliwa.

Katika ushahidi wake, Kingi ameomba mahakama ifutilie mbali kesi hiyo ya Omtatah akidai inalemaza juhudi za serikali kuinua fedha za kufadhili maendeleo.

Bunge la Seneti litawasilisha kesi kupinga Sheria ya Fedha, 2023 kupitia kwa mawakili Daniel Maanzo na Otiende Amollo.

“Tutaomba Mahakama Kuu iwasukume ndani wakugurenzi vya shirika la kidhibiti bei ya mafuta (EPRA) kwa kukaidi agizo la mahakama na kuongeza bei ya mafuta,” Bw Maanzo aliambia Taifa Leo wakati wa mahojiano maalum.

Bw Maanzo alisema maoni ya bunge la Seneti hayakushirikishwa katika Mswada wa Fedha kabla ya kutiwa saini na Rais William Ruto mnamo Juni 26, 2023.

  • Tags

You can share this post!

Mackenzie aomba mlo spesheli kizuizini

Maiti bila kichwa na mikono yapatikana katika shamba la...

T L