• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 10:50 AM
Mabawabu watatu wakana wizi wa vifaa kutoka hospitali

Mabawabu watatu wakana wizi wa vifaa kutoka hospitali

Na RICHARD MUNGUTI

WALINZI watatu wameshtakiwa kuiba vifaa vya elektronik katika hospitali inayoshughulikia magongwa ya watoto eneo la Kilimani Nairobi.

Mabawabu hao Dominic Okioma Manduku, Samson Ondieki na Martin Wamola walikanusha mashtaka mawili ya wizi na kushindwa kuzuia uhalifu ukitekelezwa mbele ya hakimu mwandamizi Bw Peter Mutua. Bw Mutua alifahamishwa na upande wa mashtaka thamani ya vifaa hivyo ni Sh221,500.

Mabawabu hao walikana kuiba kamera muundo wa Nikon iliyo na thamani ya Sh131,500, Mashine ya kupima magonjwa bei yake ni Sh56000 na Projekta ya thamani ya Sh34,000. Hakimu alielezwa vifaa hivyo vilikuwa vimefungiwa ndani ya Kiliniki hicho vilipoibwa.

Washtakiwa walidaiwa walishindwa kutumia uwezo walio nao kuzuia wizi ukitekelezwa. Meneja wa Kiliniki hicho alifungia vifaa hivyo katika afisi yake lakini hakuvipata alipoanza kufanya kazi Desemba 24,2021. Bw Mutua alifahamishwa polisi wanaendelea kuvisaka.

Kesi itatengewa siku ya kusikizwa wakati wa siku kuu ya wapendanao almaarufu Valentine inayosherehekewa Feburuari 14,2022 Kila mmoja alipewa dhamana ya pesa tasilimu Sh100,000.

You can share this post!

Mfungwa akiri kumlaghai mwanamke Sh0.8Milioni kumsaidia...

Kesi ya Willie Kimani yakamilishwa baada ya kusikizwa miaka...

T L