• Nairobi
  • Last Updated May 20th, 2024 6:55 PM
Madereva wa masafa marefu kugomea agizo wasome upya

Madereva wa masafa marefu kugomea agizo wasome upya

NA JESSE CHENGE

CHAMA cha Madereva na Makondakta wa Malori ya Masafa Marefu (LODDCA) kwa ushirikiano na Chama cha Madereva Kenya (KDA) kinatishia kuandaa mgomo wa madereva kote nchini kuanzia Julai 1 kulalamikia agizo la serikali kuwa warudi shule kufunzwa upya.

Mwenyekiti wa LODDCA, Bw Elijah Nyaga, alisema serikali kupitia Mamlaka ya Kitaifa ya Uchukuzi na Usalama inapanga kuwatoza madereva wote ada ya Sh1,050 ili kupata mafunzo hayo.

“Tuko hapa Busia kulalamika kuhusiana na maelekezo yaliyotolewa na NTSA kuhusu madereva kurudi shuleni,”alisema Elijah

Madereva hao wametoa wito kwa Waziri wa Barabara na Uchukuzi, Bw Kipchumba Murkomen kusitisha agizo la NTSA mara moja na kutoa fursa ya mazungumzo.

“Sisi lazima tuhusishwe katika masuala na mipango ya serikali ili tufanye kazi kwa pamoja,”alisema Bw Nyaga Madereva hao pia wanataka Wizara izuie madereva kutoka nchi jirani ambao wanapita barabara za Kenya bila stakabadhi halali.

“Tuna madereva wenzetu kutoka nchi nyingine ambao hawana stakabadhi za kuendesha magari katika barabara ilhali serikali ya Kenya inawaacha wahudumu,”alisema Bw Nyaga.

Wanasema hii imesababisha madereva wengi wa lori nchini Kenya kukosa kazi, ilhali wana stakabadhi sahihi za kuhudumu.
Nyaga ambaye aliandamana na Dennis Masinde ambaye ni mwenyekiti wa Chama cha MAdereva wa Kenya (KDA) anasema ikiwa serikali, kupitia Wizara ya Uchukuzi, haitachukua hatua kufikia Julai 12, 2023, wataendelea na mgomo huo kote nchini.
  • Tags

You can share this post!

Wabunge wamwidhinisha mke wa Chebukati kuwa Mwenyekiti wa...

Muuzaji magari asema alimpiga polisi kumpa funzo

T L