• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 2:24 PM
Mshukiwa wa mauaji ya afisa wa Kilifi kuzuiliwa siku 14

Mshukiwa wa mauaji ya afisa wa Kilifi kuzuiliwa siku 14

NA MAUREEN ONGALA

HAKIMU Mwandamizi Mkuu wa Kilifi Justus Kituku amewaruhusu polisi kumzuilia mshukiwa Diana Naliaka almaarufu Sarah Nekesa Barasa kwa siku 14 katika kituo cha polisi cha Kilifi.

Kiongozi wa mashtaka Bi Winnie Atieno Otieno ameiomba mahakama muda zaidi wa kumzuilia Naliaka, ambaye ndiye mshukiwa mkuu wa mauaji ya Afisa Mkuu wa Uchumi wa Baharini katika Kaunti ya Kilifi marehemu Rahab Karisa.

“Nimesikiliza ombi la kiongozi wa mashtaka kuomba muda zaidi kumzuilia mshukiwa ili kukamilisha uchunguzi wao. Sina pingamizi kwa hilo nikizingatia uzito wa kesi hiyo,” akasema hakimu Kituku.

Diana Naliaka almaarufu Sarah Nekesa Barasa ambaye ni mshukiwa wa mauaji ya Afisa Mkuu wa Uchumi wa Baharini katika serikali ya Kaunti ya Kilifi marehemu Rahab Karisa, asindikizwa na polisi kuingia katika mahakama ya Kilifi mnamo Julai 27, 2023. PICHA | MAUREEN ONGALA

Rahab aliuawa kwa kudungwa kisu nyumbani mnamo Alhamisi, Julai 20, 2023.

Inadaiwa mtafaruku ulitokea baada ya yeye kurejea nchini kutoka Italia alikohudhuria mkutano muhimu wa kimataifa na akapata pesa zake kiasi fulani zilikuwa zimepotea nyumbani.

Mshukiwa Naliaka alikamatwa katika eneo la Misikhu akitembea kwa miguu akiwa na lengo la kuingia nchini Uganda. Afisa wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai katika Kaunti ya Kilifi Bw David Siele alithibitisha kwamba mshukiwa alikamatwa mnamo Jumanne saa kumi alfajiri akipanga kutorokea katika taifa jirani.

Kesi dhidi ya mshukiwa itatajwa Agosti 17, 2023.

  • Tags

You can share this post!

Mbunge ataka somo la elimu ya masuala ya uzazi liwe la...

Soccer Assassins wawanyoa Solasa Queens bila maji

T L