• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 10:15 PM
Soccer Assassins wawanyoa Solasa Queens bila maji

Soccer Assassins wawanyoa Solasa Queens bila maji

NA TOTO AREGE

SOCCER Assassins waliwanyorosha Solasa Queens bila huruma, kwa kuwapiga 5-1 kati mechi ya Zoni B ya Ligi Kuu ya Wanawake ya Divisheni ya Kwanza mnamo Jumatano.

Mechi hiyo ya raundi ya 21, ilisakatwa katika uwanja wa Chambiti Primary mjini Luanda, Kaunti ya Vihiga.

Mshambulizi wa Assasins Charity Midewa alicheka na wavu mapema kipindi cha kwanza,  kabla ya Valarie Nekesa  kufunga mabao manne dakika ya 43’, 55’, 76’na 86.

Nekesa ndiye mfungaji bora Zoni B akiwa na mabao 25.

Bao la pekee la Solasa lilipachikwa wavuni na Joan Onyuna kunako dakika ya 17.

Assassins wamesalia nafasi ya nne na alama 45 sawa na Kisped Queens lakini wanatofautiana kwa idadi ya mabao. Wana alama tatu nyuma ya vinara wa ligi Bungoma Queens.

Kocha wa timu ya Soccer Assassins Nickson Muleri hakuficha furaha yake baada ya ushindi huo.

“Lengo letu kwenye mechi hii lilikuwa, kucheza mpira kwa kasi na kutowapa wapinzani nafasi ya kutulia. Ujuzi huu uIlitekelezwa kikamilifu na kusababisha bao letu la mapema,” alisema Muleri.

“Wapinzani pia walijibu kufanya mashambulizi lakini walishindwa. Wachezaji wetu walijua umuhimu wa mechi hii. Tulifanya mabadiliko ya kiungo wakati wakati wakati wa mapumziko na tukaleta kiungo mkabaji zaidi. Hili liliwafanya wapinzani wetu kuzidiwa maarifa zaidi,” aliongezea Muleri.

Ushindi huo, umefufua matumaini yao ya kujiunga na Ligi Kuu ya Wanawake nchini (KWPL) msimu ujao.

Solasa nao wako kwenye hatari ya kushuka daraja katika nafasi ya tisa na alama 18. Wamecheza mechi 21, wakapata ushindi mara sita, sare tatu na  kupoteza mechi 12.

Raundi ya mwisho ya mechi za msimu wa 2022/23 itachezwa wikendi hii.

Kibera Soccer Women ya Zoni B ndio timu ya pekee ambayo imejiunga na KWPL.

  • Tags

You can share this post!

Mshukiwa wa mauaji ya afisa wa Kilifi kuzuiliwa siku 14

Wito wa utangamano na amani Rais Ruto akizuru Lamu

T L