• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 12:18 PM
Mwamko mpya mahakama ya Thika ikipata jaji

Mwamko mpya mahakama ya Thika ikipata jaji

NA LAWRENCE ONGARO

MAHAKAMA ya Thika imepanda ngazi na kupata jaji ikitarajiwa kwamba kesi zilizorundikana huko zitasikilizwa na kuamuliwa upesi.

Jaji Florence Muchemi aliyefika kuchukua usukani Thika alisema ataharakisha kesi zilizorundikana katika Mahakama Kuu ya Thika.

Akihutubia waandishi wa habari katika afisi yake jaji Muchemi alisema kesi 535 ambazo zilipelekwa katika mahakama ya Kiambu sasa zitasikilizwa Thika.

“Tayari tumeanza kazi rasmi na nina uhakika tutafanya juhudi kukamilisha kesi hizo haraka iwezekanavyo,” alisema jaji Muchemi.

Alizungumzia mafanikio ya kesi  539 za mfumo wa kidijitali (e-filing) ambazo zinaendeshwa kupitia mtandao.

Alisema kutakuwa na mabadiliko makubwa baada ya mahakama ya Thika sasa kupata jaji.

Alisema kutakuwepo na kesi za kuendeshwa kimtandao na zile za kawaida katika mahakama hiyo.

Alisema kesi zinazohitaji kuwa na mashahidi na kutoa ushahidi zitaendelea kama kawaida katika mahakama ya Thika.

Hata hivyo, alipendekeza mahakama ya Thika iwe na eneo kubwa ili kutosheleza pahala pa kuhifadhi faili za kesi zinazowasilishwa mahakamani.

Kulingana na mpangilio uliopo sasa, kesi kubwa za kutoka kaunti ndogo za Thika Mjini, na Ruiru zitawasilishwa katika mahakama ya Thika.

  • Tags

You can share this post!

Kampuni yalia wanyakuzi wa ardhi ya kingo za mto Ngong...

Lami: Hatimaye Lamu Mashariki yafikiwa

T L