• Nairobi
  • Last Updated May 9th, 2024 1:42 PM
Naisula Lesuuda kati ya wabunge 10 bora wa kike wanaochapa kazi sambamba

Naisula Lesuuda kati ya wabunge 10 bora wa kike wanaochapa kazi sambamba

NA MARY WANGARI

JUMLA ya wabunge sita wanawake wameorodheshwa miongoni mwa wabunge 10 wachapakazi kitaifa katika kaunti mbalimbali.

Mbunge wa Samburu Magharibi, Kaunti ya Samburu, Josephine Naisula Lesuuda, anaongoza orodha hiyo ya viongozi wa kike wachapakazi huku akiwa pekee aliyeorodheshwa miongoni mwa wabunge 10 wachapakazi kitaifa.

Katika utafiti uliofanywa na kampuni ya Infotrak, Bi Lesuuda aliibuka nambari tano kitaifa baada ya kujizolea asilimia 63.

Mbunge wa Mwea, Mary Maingi aliibuka wa pili katika kaunti hiyo kwa asilimia 52.

Katika Kaunti ya Nakuru, mbunge wa Bahati Irene Njoki aliibuka wa kwanza akifuatwa unyounyo na mwenzake wa Gilgil Martha Wangari katika nafasi ya tatu.

Wanawake katika Kaunti ya Uasin Gishu walitamba katika uchapaji kazi, mbunge wa Turbo, Janet Sitienei na mwenzake wa Moiben, Phyllis Jepkemoi, wakijizolea nafasi ya kwanza na ya pili mtawalia.

Mbunge wa Laikipia Kaskazini Sarah Paulata pia aling’aa.

 

  • Tags

You can share this post!

Wafugaji Nakuru walalamikia nyani kunyonya maziwa ng’ombe...

Penzi la mauti: Mume katili alivyoangamiza mke kwa kumdunga...

T L