• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 10:50 AM
Nyakati ngumu makundi mengi yakishindwa kulipa mikopo ya Uwezo Fund

Nyakati ngumu makundi mengi yakishindwa kulipa mikopo ya Uwezo Fund

NA KASSIM ADINASI

MAKUNDI ya Watu Walemavu (PWDs) katika kaunti ndogo ya Ugunja yamemulikwa kwa kushindwa kulipa mikopo kutoka kwa hazina ya Uwezo Fund.

Tangu kuanzishwa kwa hazina hiyo mwaka 2014, makundi matano ya PWDs yamenufaika katika eneo hilo lakini hakuna hata kundi moja lililolipa mkopo.

“Hali ni ngumu kwetu kwa sababu hizi ni pesa za mzunguko,” akasema Bw Ainea Ayamba, ambaye ni Mwenyekiti wa Uwezo Fund kaunti ndogo ya Ugunja.

Amewataka wanachama wa makundi hayo kufahamu kwamba pesa za uwezo si za ruzuku bali ni mkopo bila riba.

“Mara nyingi tunakopesha kikundi takriban Sh100,000 kwa mara ya kwanza. Wakilipa ndipo kiwango kinapanda,” akasema.

Pia amesuta makundi ya vijana kwa ulegevu.

“Kati ya 50 ni makundi sita tu ya vijana ambayo yamekuwa yakilipa na kuongezewa mikopo. Hayo mengine hayajalipa na hali hii inafanya iwe vigumu kutoa mikopo kwa makundi mengine,” akasema Bw Ayamba.

Lakini kwa upande mwingine, makundi ya akina mama yanafanya vyema ambapo 310 yamenufaika tangu kuanzishwa kwa Uwezo fund.

Bi Lilian Kinuthia, ambaye ni afisa kutoka Sekritariati ya Uwezo Fund anasema hazina hiyo imebadilisha maisha ya wengi.

“Makundi mengi yamenufaika na mikopo ya Uwezo Fund na wanawake wengi wanaendesha biashara zao katika maeneo mbalimbali ya nchi,” akasema Bi Kinuthia.

Katika eneobunge la Ugunja, jumla ya Sh40 milioni zimekopeshwa kwa makundi 373.

Mbali na makundi hayo, pia vyama vya ushirika – SACCOs – vinane vimenufaika katika eneobunge hilo la Ugunja.

[email protected]

  • Tags

You can share this post!

Ruto awapongeza wanajeshi wa KDF kwa kulinda nchi dhidi ya...

Wanawake wazungu wanatupenda sababu tuna nyama ya ulimi,...

T L