• Nairobi
  • Last Updated May 21st, 2024 8:55 PM
Rais Ruto aonya wawekezaji dhidi ya kuacha ardhi kwa muda mrefu bila ustawishaji

Rais Ruto aonya wawekezaji dhidi ya kuacha ardhi kwa muda mrefu bila ustawishaji

NA LABAAN SHABAAN

RAIS William Ruto ameamuru Wizara ya Ardhi ibatilishe hatimiliki za mashamba ambayo hayajastawishwa huko Athi River kwa muda wa zaidi ya miaka 10.

Kiongozi wa nchi alilenga wastawishaji wanaohodhi mashamba bila kuyatumia alipozungumza katika uzinduzi wa Kampuni ya Kuzalisha Dawa ya Square (Square Pharmaceuticals PLC) iliyoko Athi River, Kaunti ya Machakos.

“Nimetoa maagizo wazi kwa usimamizi hapa kuwa, wakisiaji wote walio na hatimiliki za ardhi kwa miaka 10, 15, 20, 30 bila kutumia, zinafaa kubatilishwa ili mashamba yatolewe kwa watu wanaotaka kutumia kiwanda hiki,” aliamuru.

Kadhalika, Rais Ruto aliamuru ardhi ya ekari 1,000 iliyoibwa kutoka kwa Kampuni ya Saruji ya East Africa Portland Cement Company (EAPCC) ipelekwe kwa eneo la Nchi za Nje (EPZ).

Oktoba 9, 2023, korti ilitoa uamuzi kuwa shamba hilo la ekari 4,298 linamilikiwa na EAPCC baada ya mgogoro wa zaidi ya mwongo mmoja na maskwota.

Amri hii inatarajiwa kupingwa na maskwota ambao wamekuwa wakivutana na kiwanda hicho cha saruji kwa miaka.

“Naarifiwa kuna shamba la ukubwa wa ekari 250 ambalo lilimilikiwa na wakisiaji na tunaweza kuleta ardhi zaidi katika kiwanda cha EPZ, Athi River,” Dkt Ruto aliongeza akisema kuna haja ya kuongeza kampuni zaidi Kenya ili kufanikisha ustawi wa kiviwanda.

Serikali inasema kuwa inajizatiti kuongeza maeneo maalum ya kiuchumi Thika, Eldoret, Busia na Nakuru katika awamu ya kwanza.

Kupitia mpango huu, serikali inatazamia kuvutia wawekezaji watakaokita biashara zao na kustawisha uchumi wa nchi.

  • Tags

You can share this post!

Kasisi wa Afrika Kusini anayeacha mabinti wa Kenya na kiu...

Martial wa Man United atema visura wawili, aoga na kurudi...

T L