• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 7:55 AM
Kasisi wa Afrika Kusini anayeacha mabinti wa Kenya na kiu ya mahaba

Kasisi wa Afrika Kusini anayeacha mabinti wa Kenya na kiu ya mahaba

NA MERCY KOSKEI

KASISI mmoja kutoka Afrika Kusini amezua msisimko nchini, kutokana na video zake kwenye mtandao wa TikTok zinazomuonyesha akicheza na kujiburudisha wakati wa misa.

Kasisi huyo kwa jina Karabo Lephuthing, almaarufu @karabopapak kwenye TikTok, amewavutia watazamaji wa Kenya kwa sura yake nzuri na kontenti anayochapisha.

Video hizo, zinaonyesha Karabo akicheza kwa sauti maarufu za TikTok na kufuraia wakati wa misa, jambo ambalo limewasisimua wanamitandao hasa wanawake wa Kenya.

Mwanakontenti wa TikTok kwa jina Risper Njeri, alichapisha video ya kasisi huyo akiimba kwa utani wimbo maarufu wa Kikatoliki “Twende sote nyumbani mwake” akisema kuwa yuko tayari kuhudhuria misa inayoongozwa naye.

Video hiyo ilivutia sana Wakenya ambao walikuwa na shauku ya kutaka kujua kasisi huyo alikuwa nani na alitoka wapi.

Hili lilizua tafrani miongoni mwa Wakenya, ambao walipata akaunti ya TikTok ya kasisi huyo na kuanza kueleza hisia zao kwa mtumishi huyo wa Mungu.

Wanawake wa Kenya wamekuwa wakimiminika kwa wingi katika akaunti ya Karabo ya TikTok, wakionyesha mapenzi yao kwa kasisi huyo.

Wengine wamefikia hatua ya kueleza nia yao ya kusafiri hadi Afrika Kusini ili kuhudhuria ibada ya misa kwenye kanisa hilo.

Wengi walifurika kwenye safu ya maoni, kutoa hisia zao tofauti huku wakipendekeza kwa mzaha kuwa watawasiliana na Rais William Ruto ili amwalike Papa aje kuwabariki waumini wa Kenya.

Sonnie, alisema, “Ruto tunahitaji mtu huyu wa Mungu kuwaombea wanawake wetu na tunaahidi tutabadilika kabisa.”

Abby@123 pia alitoa maoni, “Kwa heshima zote mtu wa Mungu unaweza kufanya misa takatifu katika uwanja wa Kasarani, kwani tunakuhitaji ufanye muujiza nchini Kenya ? lakini tunafanya mchanganyiko.”

  • Tags

You can share this post!

Maduka yaanza kukataa ‘Lipa Na Mpesa’ sababu ya ushuru...

Rais Ruto aonya wawekezaji dhidi ya kuacha ardhi kwa muda...

T L