• Nairobi
  • Last Updated April 17th, 2024 6:55 PM
Ruto ammegea Echesa mnofu serikalini

Ruto ammegea Echesa mnofu serikalini

NA CHARLES WASONGA

HATIMAYE Waziri wa zamani wa Michezo Rashid Echesa ametunukiwa cheo katika serikali ya Kenya Kwanza.

Rais William Ruto amemteua kuwa mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Kusimamia Chemichemi za Maji Nchini, (Kenya Water Towers Agency Board).

“Miye, William Samoei Ruto, Rais wa Kenya na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi yote ya Ulinzi namteua Rashid Echesa kuwa mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Chemichemi za Maji Nchini kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia Mei 19, 2023,” ikasema notisi ya gazeti rasmi la serikali toleo la Mei 18, 2023.

Rais Ruyo alifutilia mbali uteuzi wa Bw Robert M Kariuki, aliyeteuliwa na Rais mstaafu Uhuru Kenyatta.

Bw Echesa, ambaye aliwania kiti cha ubunge cha Mumias Magharibi 2022 na kushindwa na Johnston Naicca wa ODM,  amekuwa mwandani wa karibu zaidi wa Rais Ruto kutoka Kaunti ya Kakamega.

Bw Echesa alipigwa kalamu na Bw Kenyatta mnamo Machi 2019 na nafasi yake ikachukuliwa na Balozi Amina Mohamed.

  • Tags

You can share this post!

Rachel Hellen Waithira: Siri ya mafanikio ni kujua...

CECIL ODONGO: Raila aingilie kati na kuzima uhasama kati ya...

T L