• Nairobi
  • Last Updated December 5th, 2023 10:25 PM
Ruto amwondoa Haji kama DPP

Ruto amwondoa Haji kama DPP

Na RICHARD MUNGUTI

RAIS William Ruto amemteua Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka ya Umma (DPP) Noordin Haji, kuwa mkurugenzi mpya wa Idara ya Ujasusi (NIS).

Iwapo bunge la kitaifa litamwidhinisha Bw Haji, atachukua wadhifa huo kutoka kwa Meja Jenerali Mstaafu Philip Wachira Kameru anayetarajiwa kusaafu.

Mtaalam huyo wa masuala ya sheria na ujasusi alimrithi wakili mwenye tajriba ya Keriako Tobiko mnamo Machi 2018.

Kipindi cha Haji kama DPP kimekumbwa na patashika nyingi.

Haji alipata Shahada ya Digirii ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Wales.

Kulikuwa na kesi nyingi za kuomba atimuliwe kazini kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake.

  • Tags

You can share this post!

LISHE: Fahamu mbona unahimizwa kula mboga za kijani

MAPISHI KIKWETU: Mchicha

T L