• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 5:50 AM
Ruto: Ziara yangu Nyanza ni makusudi kuondoa ukasumba wa ubaguzi

Ruto: Ziara yangu Nyanza ni makusudi kuondoa ukasumba wa ubaguzi

NA SAMMY WAWERU

RAIS William Ruto amesema Jumapili, Oktoba 8, 2023 kwamba ziara yake eneo la Nyanza ni ya makusudi inayolenga kupeleka maendeleo ‘katika eneo ambalo kwa muda mrefu limelalamikia kubaguliwa’.

Akizungumza katika Taasisi ya Mafunnzo ya Ualimu ya Uriri, Migori ambapo alishiriki ibada ya pamoja ya misa, Dkt Ruto alisema hakuzuru Nyanza kwa sababu hana maeneo mengine kuenda.

“Kuja kwangu Migori hakumaanishi sina mahali kwingine kwa kuenda…Nimekuja Nyanza kimakusudi ili kuondoa kasumba ya muda mrefu kuwa eneo hili limetengwa kimaendeleo,” Rais Ruto akasema.

Alisema kuchaguliwa kwake Agosti 2022 kuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Kenya, kuliashiria mwisho wa siasa za kikabila.

Chini ya utawala na uongozi wake, Rais Ruto alisema kila eneo nchini lazima lipate minofu ya serikali – maendeleo.

“Uchaguzi uliopita, mambo yalikuwa matatu; Amani, kuondoa sera za ukabila na kwa mara ya kwanza Kenya, wananchi na Mungu walichagua kiongozi wao, wala si wa mtambo, ama wa mateka wa ‘serikali’,” akaelezea.

Katika uchaguzi wa 2022, Dkt Ruto (Kenya Kwanza) alimenyamana na kinara wa Azimio la Umoja, Bw Raila Odinga, na alimshinda kwa zaidi ya kura 200, 000.

Nyanza kwa muda mrefu imekuwa ikilalamikia kubaguliwa kimaendeleo, na Rais Ruto katika ziara yake ya siku kadha eneo hilo amezindua miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa nyumba za bei nafuu, babarabara, vituo vya afya, miongoni mwa mingine.

 

  • Tags

You can share this post!

Kalonzo awatetea Mutua na Malonza kwa kushushwa vyeo

Letoo ‘amteua’ aliyekuwa mume wa Akothee kuwa...

T L