• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 7:50 PM
Letoo ‘amteua’ aliyekuwa mume wa Akothee kuwa Katibu Mkuu wa Masuala ya Nchi za Kigeni

Letoo ‘amteua’ aliyekuwa mume wa Akothee kuwa Katibu Mkuu wa Masuala ya Nchi za Kigeni

NA SAMMY WAWERU

MWANAMUZIKI maarufu, Esther Akoth, anayejulikana kama Akothee, anaendelea kuwa gumzo la mitandao ya kijamii, wasanii na hata watangazaji tajika wakitoa maoni yao hasa baada ya tangazo lake hivi majuzi kutengana na mumewe, Denis Schweizer.

Mtangazaji Stephen Letoo, ambaye amejitawaza ‘Rais’ wa Baraza la Muungano wa Wanaume, ndiye wa hivi karibuni kutoa tamko na hisia kuhusu tangazo la Akothee.

Kupitia ukurasa wake rasmi wa Facebook, katika chapisho la kutania Bw Letoo alitangaza uteuzi wa aliyekuwa mume wa mwanamuziki huyo kuwa ‘Katibu Mkuu wa Masuala ya Nchi za Kigeni”.

Alisema alitoa uamuzi huo kutokana na mamlaka aliyopewa kama ‘Rais’ wa Baraza la Muungano wa Wanaume.

“MABADILIKO KATIKA BARAZA LA WANAUME: Kwa mamlaka niliyopewa kama Rais wa Baraza la Muungano wa Wanaume, chini ya Kifungu 2A, ninafanya mabadiliko yafuatayo; 1. Bw Denis Schweizer (Omosh) ameteuliwa rasmi kuwa Katibu Mkuu wa Masuala ya Nchi za Kigeni,” aliandika mwanahabari huyo wa masuala ya kisiasa katika runinga ya Citizen.

Akothee alikuwa ameolewa na Schweizer, ambaye alimtambua kwa jina la utani kama ‘Omosh’.

Katika chapisho hilo la Ijumaa, Oktoba 6, 2023 Letoo pia aliambatanisha picha ya mume aliyetengana na mwanamuziki huyo, akipanda farasi.

Aidha, picha hiyo ilipigwa wakati wa harusi ya kifahari ya Akothee Aprili 2023 na raia huyo wa Uswisi.

“Mwenye ofisi hiyo kwa sasa amerejeshwa Nairobi, Kenya. Mabadiliko zaidi yatafuata…!” linasema chapisho la kuchekesha la Letoo, ambalo limezua ucheshi mitandaoni.

Letoo alijitawaza kuwa ‘Rais’ wa Baraza la Muungano wa Wanaume mwanzoni mwa 2023 wakati wa hafla aliyoiandaa.

Tangu wakati huo, amekuwa akizungumzia masuala yanayohusiana na wanaume, kutoa mwongozo, na ushauri nasaha.

Majuzi, Akothee alitangaza kutengana na mumewe kwa sababu ambazo hazikufichuliwa, alizoahidi kueleza siku zijazo.

Alichapisha kwenye ukurasa wake rasmi wa Facebook, akikiri kuwa anaendelea kupata nafuu kutokana na msongo wa Mawazo.

Aliandika, “Niruhusu niwashukuru wote waliokuwa wakiniombea kimya kimya, kila mtu aliyeniongoza katika safari hii. Nimetoka hatarini, na nimekuwa nikipona kisirisiri.”

“Nipo katika mwezi wangu wa pili wa tiba, nikipambana na msongo wa mawazo nilioupata baada ya kugundua ukweli na mambo mabaya ambayo yalinishtua,” alisema mwanamuziki huyo.

  • Tags

You can share this post!

Ruto: Ziara yangu Nyanza ni makusudi kuondoa ukasumba wa...

Akothee atishia kuzua fujo kwenye benki baada ya pesa zake...

T L