• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 10:55 AM
Serikali kutoa ‘data bundles’ za bure kwa watakaonunua simu alizozindua Rais Ruto

Serikali kutoa ‘data bundles’ za bure kwa watakaonunua simu alizozindua Rais Ruto

NA CHARLES WASONGA

WIZARA ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) imetoa zawadi ya ‘data bundles’ bila malipo kwa Wakenya watakaonunua simu aina ya smartphone za bei rahisi zilizozinduliwa wiki jana na Rais William.

Katibu katika Wizara hiyo Mhandisi John Tanui alisema kuwa hatua hiyo inalenga kuwatia shime Wakenya kununua simu hizo, moja ikiuzwa kwa bei ya Sh7,499.

Azma ya serikali ni kustawisha uchumi wa kidijitali.

“Serikali inalenga kuhakikisha kuwa Wakenya wanakumbatia mfumo wa kuendesha shughuli za kiuchumi kidijitali. Kwa kutumia simu hizi, wananchi watapata nafasi kupata zaidi ya huduma 5,000 ambazo wakati huu zinapatikana kupitia mitandao,” akasema Bw Tanui.

“Simu hizi zilizozinduliwa juzi na Mheshimiwa Rais Ruto zinagharimu Sh7,499 pekee na wanunuzi wa kwanza kwanza watapewa ‘bundles’ bila malipo,” Bw Tanui akasema Jumatano asubuhi kwenye mahojiano katika kituo cha redio cha Spice FM.

Hata hivyo, Katibu huyo wa Wizara hakufichua kiwango cha data ambacho wanunuzi wa kwanza wa simu hiyo watapewa.

“Wakati huu uchumi wa kidijitali unakuwa mara 2.5 ya uchumi wa kawaida. Hii ndiyo maana serikali imejitolea kuendeleza uchumi huu kwa kuzindua simu hizi ambazo zitahakikisha kuwa hata Wakenya katika maeneo ya mashambani wanapata huduma za serikali kwa urahisi,” Bw Tanui akakariri.

Mnamo Oktoba 30, 2023 Rais Ruto alizindua simu hiyo mpya inayotengenezwa na kampuni ya kampuni ya East Africa Device Assembly Kenya (EADAK) Ltd, iliyoko eneo la Mavoko, Kaunti ya Machakos.

Rais William Ruto (kulia) akiwa kwa kiwanda cha kutengeneza simu kilichoko Mavoko. PICHA | PCS

Simu hizo chapa Neon 5 ‘Smarta’ na 6 ½ ‘Ultra’  zina uwezo wa kutumia mawimbi ya 4G na zinauzwa katika maduka ya Faiba, maduka ya Safaricom na maduka mengine ambayo huuza simu kote nchini.

Aidha, zitauzwa mitandaoni kupitia jukwaa la ‘Masoko online’.

  • Tags

You can share this post!

Jinsi waziri Kuria alivyojipalia makaa kwa kumtetea Mwangaza

Sarah Kabu atumia Sh500,000 kuipa ngozi ulaini wa kipekee

T L