• Nairobi
  • Last Updated April 12th, 2024 5:55 PM
Sarah Kabu atumia Sh500,000 kuipa ngozi ulaini wa kipekee

Sarah Kabu atumia Sh500,000 kuipa ngozi ulaini wa kipekee

NA FRIDAH OKACHI

MENEJA Mkurugenzi wa kampuni ya kutoa huduma za usafiri wa kitalii, Bonfire Adventures, Sarah Kabu ameupa uso wake mng’ao wa kipekee baada ya kulainishwa ngozi.

Sarah Kabu mwenye umri wa miaka 47 alilainishwa ngozi kupitia utaratibu wa Botox Injection procedure.

Ulainishaji huo umefanwa kwa njia ya kipekee na kumgharimu Sh500,000.

Mkurungenzi huyo alifanyiwa ‘ulainishaji’ huo katika kliniki ya Mayo, ambapo daktari mmoja wa kigeni alitoa huduma hizo jijini Nairobi.

Katika mtandao wa TikTok, Bi Kabu alichapisha video moja ambapo daktari wake anaonekana akimdunga sindano kwenye uso wake.

Mchakato huo wa akidungwa mara kadhaa sindano yenye dawa ya kuondoa makunyanzi na kulainisha ngozi ya usoni unafahamika kama ‘Botox Injection’.

“Acha tuone jinsi mambo yatakavyoenda, usiogope… unahisi vipi sasa?” aliuliza daktari huyo.

Naye Bi Kabu akajibu.

“Nilidhani ningehisi uchungu lakini kumbe si hivyo,” akajibu.

Sindano ya Botox hutumiwa kuzuia kemikali fulani kutoka kwa mishipa.

Matumizi ya dawa hiyo ikiwa ni kulegeza misuli ya uso ambayo husababisha mikunjo ya uso.

  • Tags

You can share this post!

Serikali kutoa ‘data bundles’ za bure kwa watakaonunua...

Safaricom yaponea katika kesi ya Sh305 bilioni walalamishi...

T L