• Nairobi
  • Last Updated October 2nd, 2023 8:00 AM
Upande wa mashtaka waomba Mackenzie aendelee kukaa kizuizini kwa siku 60 zaidi

Upande wa mashtaka waomba Mackenzie aendelee kukaa kizuizini kwa siku 60 zaidi

NA WACHIRA MWANGI

MHUBIRI wa kanisa la Good News International Paul Mackenzie amefikishwa katika Mahakama ya Shanzu jijini Mombasa leo Ijumaa, Juni 2, 2023. ambapo upande wa mashtaka unaomba aendelee kuzuiliwa kwa siku 60 zaidi.

Upande huo wa mashtaka unataka mhubiri huyo, mkewe na watu wengine 16 waendelee kuzuiliwa huku uchunguzi ukiendelea.

Inadaiwa Mackenzie na wenzake walipotosha waumini kufunga hadi kufariki.

Inasdaiwa waumini hao walishawishika kufunga na wakaanza kufariki miili yao ilipodhoofika.

Kufikia sasa miili ya watu zaidi ya 243 imeshafanyiwa upasuaji katika mochari ya Hospitali Kuu ya Malindi katika Kaunti ya Kilifi.

Wengi ni wale ambao miili yao iliondolewa kwenye makaburi ambayo maafisa wa usalama walipata msituni Shakahola.

  • Tags

You can share this post!

AK yaitisha mkutano na makocha wakune vichwa jinsi ya...

Omtatah awasilisha kesi kupinga Mswada wa Fedha 2023

T L