• Nairobi
  • Last Updated May 13th, 2024 7:55 AM
Ushoga: Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini Kenya wamtetea Papa Francis kwa kufafanua agizo lake

Ushoga: Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini Kenya wamtetea Papa Francis kwa kufafanua agizo lake

NA CHARLES WASONGA

KANISA Katoliki limekana madai kuwa Papa Francis ameidhinisha ndoa baina ya wapenzi ambao ni mashoga na wasagaji, wakisema kuwa ameruhusu makasisi wa kanisa hilo kuwabariki tu watu walio kwa uhusiano wa aina hiyo ambao aliurejelea kama usio wa kawaida akitumia neno ‘irregular’.

Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini Kenya (KCCB) aidha limesema kuwa agizo lililotolewa na Papa huyo lilikuwa ni la kualika mashoga kanisani “kwa matumaini kuwa watapata wokovu” na wabadili mienendo yao.

“Stakabadhi hii inalenga kualika watu wote kwa uwepo wa Mungu na neema. Kanisa Katoliki linalenga kufikia watu wote ili wapate wokovu,” mwenyekiti wa KCCB Askofu Martin Kivuva Musonde akaeleza.

Askofu Musonde alikubali kwamba watu wanashangaa ikiwa Kanisa Katoliki linaunga mkono ndoa ya wapenzi wa jinsia moja “au linabadilisha maana ya ndoa kama asasi Sakramenti ya Kanisa kati ya mwanamume na mwanamke”.

“Kila wakati Papa Francis amekuwa akiwataka Makasisi kuwa na moyo wazi kama Kanisa na kulifungua kwa wote bila kujali viwango vya maadili yao. Kanisa liwe taasisi inayowakaribisha wote, mahala ambapo wote wanahisi kukaribishwa,” akasisitiza.

“Stakabadhi ya Baba Mtakatifu inatambua kuwa wote wamealikwa kupokea baraka kutoka kwa Kanisa au Kiongozi wa Kanisa,” Askofu Musonde akaongeza.

Alieleza kuwa baraka hizo zinaweza kupewa hata wale ambao si waumini wa Kanisa Katoliki au si Wakristu na wanataka kupokea baraka za Mungu.

Askofu Musonde anasema kuwa stakabadhi hiyo haibadilishi maana ya ndoa kama kuja pamoja kwa mume na mke ili waunde familia ya kudumu.

Soma Pia: Waislamu mjini Eldoret walaani hatua ya Papa Francis kukubali wapenzi wa jinsia moja kubarikiwa

  • Tags

You can share this post!

Mwalimu asakwa akidaiwa kuwaua kwa kuwachinja wanawe wawili

Pasta asitisha injili kutimua jombi aliyesumbua akihubiri

T L