• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 1:46 PM
Wabunge kutathmini pendekezo la ‘kugatua’ Kenya Power

Wabunge kutathmini pendekezo la ‘kugatua’ Kenya Power

Na SAMWEL OWINO

BUNGE la Kitaifa linatarajiwa kuanza uchunguzi kuhusiana na bei ya juu ya umeme nchini kwa lengo la kupunguzia raia gharama ya umeme.

Kamati ya Bunge kuhusu Kawi inatarajiwa kuwasilisha ripoti yake bungeni kwa muda wa siku 120.

Miongoni mwa mapendekezo ya kupunguza bei ya umeme ambayo kamati hiyo itazingatia ni kugawanya shirika la kusambaza umeme nchini, Kenya Power, kuwa kampuni sita tofauti.

Kila kampuni itashughulikia eneo fulani la nchi. Wanakamati pia watatathmini pendekezo la kutaka mikataba ya sasa baina ya Kenya Power na kampuni za kibinafsi za kuzalisha umeme ifutiliwe mbali.

Pendekezo jingine ni kwamba Kenya Power iwe ikilipia tu umeme uliotumika.

Uchunguzi huo uliagizwa baada ya Bunge kupitsha mswada uliowasilishwa na Mwakilishi Mwanamke Laikipia, Jane Kagiri, akilenga kuzuia Wizara ya Kawi na Kenya Power dhidi ya kufanya mikataba mipya na IPPs hadi uchunguzi kuhusu bei ghali ya umeme utakapokamilishwa.

Bi Kagiri amehoji kiini cha Kenya Power kuingia kwenye mikataba ghali kushinda KenGen ambacho ni kiwanda cha serikali cha kuzalisha umeme.

Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Nancy Gathungu, katika ripoti yake kuhusu bajeti ya 2017/18 na 2020/21, anaashiria kuwa bei ya kununua umeme kati ya KenGen na wanakandarasi wa kibinafsi inaashiria kuwa inagharimu Kenya Power kiasi cha jumla ya Sh5.3 kwa kila kilowati inayonunuliwa kutoka Kengen na Sh15.3 kwa kila kilowati kutoka kwa wanakandarasi wa kibinafsi.

Katika kikao Alhamisi, Kamati hiyo ilijadili mbinu mbalimbali za kusuluhisha bei ghali ya umeme na kupendekeza kuigawanya Kenya Power kuwa kampuni mbalimbali.

“Kwa mfano, tunaweza kuwa na kampuni inayosambaza umeme katika maeneo kama vileEldoret, Busia na Siaya. Hii itaboresha utendakazi,” alisema Mbunge wa Gem, Elisha Odhiambo.

 

  • Tags

You can share this post!

Ushuru: Raila ni moto wa karatasi, adai Ruto

Wamuchomba: Nitaendelea kutetea sauti ya mnyonge licha ya...

T L