• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 10:50 AM
Wakili wa miaka 91 ashtakiwa kwa wizi wa Sh63.7 milioni  

Wakili wa miaka 91 ashtakiwa kwa wizi wa Sh63.7 milioni  

Na RICHARD MUNGUTI
WAKILI mkongwe mwenye umri wa miaka 91 ameshtakiwa kwa kuiba Sh63 milioni alizokuwa anahifadhi kwa niaba ya familia ya mtu na mkewe waliokufa.

Akram Mohamed Khan alipokea pesa hizo baada ya kuuza shamba la marehemu Sukhdev Singh Mangat.

Akipokea ushahidi katika kesi hiyo inayomkabili Khan, hakimu mkuu mahakama ya Milimani Lucas Onyina alielezwa polisi hawakupata hata senti moja katika akaunti ya mshtakiwa.

Khan ameshtakiwa kwa kuiba Sh63, 700, 000 alizopokea kwa niaba ya marehemu Sukhdev Singh Mangat.

Onyina alifahamishwa mshtakiwa aliiba pesa hizo akishirikiana na watu wengine ambao hawakufikishwa kortini.

Shtaka lasema alitekeleza wizi huo kati ya Desemba 4, 2013 na Septemba 16, 2014 katika Benki ya Habib tawi la Koinange, jijini Nairobi.

Uchunguzi uliofanywa na polisi haukuzaa matunda kwa vile hawakupata hata hela moja kutoka kwa Khan.

Khan alikuwa amekawia kushtakiwa kutokana na changamoto za kiafya.

Kibali cha kumtia nguvuni kilitolewa na aliyekuwa hakimu mkuu Wendy Kagendo.

Mthamini wa mali ya marehemu aliyetoa ushahidi alieleza korti pesa hizo Sh63.7 milioni ziliuzwa shamba iliyoko Kisumu.

Shamba hilo lilinunuliwa na Surgit Sigh na Malkit Sigh kwa bei ya Sh63 milioni.
Asilimia 10 ya pesa hizo Sh6.3 milioni zililipwa Khan mnamo Machi 15 2014.

 

  • Tags

You can share this post!

MAPISHI KIKWETU: Pancakes zilizojazwa nyama

BORESHA AFYA: Vitamu visivyoleta madhara mwilini

T L