• Nairobi
  • Last Updated May 6th, 2024 8:55 PM
BORESHA AFYA: Vitamu visivyoleta madhara mwilini

BORESHA AFYA: Vitamu visivyoleta madhara mwilini

NA MARGARET MAINA

[email protected]

KWA upande mmoja, pipi na kitindamlo kitamu lakini kwa upande mwingine, huwa na sukari nyingi na kalori tupu.

Wataalamu wa afya wanashauri kwamba ni muhimu kwa mtu kupunguza sukari iliyoongezwa, kama vile pipi, kwa sababu inaweza kuwa na madhara kwa afya kwa kuongeza uvimbe na kuongeza hatari ya ugonjwa wa moyo na na matatizo ya mishipa, kutaja tu machache.

Habari njema ni kwamba inawezekana kukidhi tamaa ya vitu vitamu bila kutumia pipi ambazo zinaongezwa sukari na kalori tupu.

Basi ikiwa unatamani kitu kitamu lakini hutaki kilete madhara, hapa kuna orodha ya kukusaidia kufanya uamuzi wa busara.

Pipi zenye afya

Ni nini kinachoweza kufanya kitindamlo na pipi kuwa za manufaa kiafya? Kando na kupunguza sukari iliyoongezwa, yafuatayo ni mambo ya kawaida kwa pipi zenye afya.

Kutokana na matunda

Pipi zenye afya hutumia matunda kama kitamu asilia – si sharubati ya matunda au ladha ya matunda bali matunda halisi. Kwa mfano, peremende nyingi zenye afya hutumia tende kama kiungo kwa sababu ni tamu.

Kutumia tende au matunda mengine kunaweza kupunguza hitaji la sukari nyingine yoyote inayohitajika.

Beri na tufaha ni matunda mengine mazuri yanayotumika kutengeneza pipi salama kwa afya ya mwanadamu. Kitindamlo bora ni kile kisicho na sukari iliyoongezwa.

Chanzo cha protini au mafuta yenye afya

Mbali na utamu, pipi zenye afya huwa na protini na/au mafuta yenye afya ambayo huongeza thamani ya lishe. Virutubisho hivi pia husaidia kuweka sukari kwenye damu kuwa thabiti baada ya kula badala ya kupeleka sukari kwenye damu na pia husaidia mtu ajisikie ameshiba baada ya kula.

Baadhi ya vyanzo vya protini na mafuta kwa kitindamlo vinaweza kujumuisha:

  • karanga / mbegu / siagi ya karanga
  • mtindi au jibini
  • shayiri
  • njegere
  • mafuta ya mzeituni au parachichi
  • kwinoa
  • kakao

Viungo vichache vilivyochakatwa kupita kiasi

Viungo vikuu vya kusindikwa katika pipi na kitindamlo ni sukari nyeupe na unga mweupe. Vyakula hivi vina wanga kwa wingi na havina thamani ya lishe. Kwa hivyo, ni muhimu kupunguza sukari na wanga wakati wa kula pipi zenye afya.

Vyanzo mbadala vya sukari nyeupe katika kitindimlo bora vinaweza kuwa vitamu vingine kama vile asali, sukari ya nazi, na sharubati safi ya mshira. Vyanzo mbadala vya unga mweupe ni unga wa shayiri, unga wa mlozi, au unga wa ngano.

  • Tags

You can share this post!

Wakili wa miaka 91 ashtakiwa kwa wizi wa Sh63.7 milioni  

BORESHA AFYA: Fahamu umuhimu wa cheri

T L