• Nairobi
 • Last Updated May 22nd, 2024 6:07 PM
MAPISHI KIKWETU: Pancakes zilizojazwa nyama

MAPISHI KIKWETU: Pancakes zilizojazwa nyama

NA MARGARET MAINA

[email protected]

Muda wa kuandaa: Dakika 15

Muda wa mapishi: Dakika 20

Walaji: 3

Vinavyohitajika

 • vitunguu maji 2 vilivyokatwa
 • nyanya 3 zilizotolewa ngozi ya juu halafu zikakatwa
 • majani ya giligilani
 • pilipili ya kijani kipande 1
 • chumvi
 • mayai 2
 • maji baridi
 • nyama ya ng’ombe/kuku iliyosagwa
 • unga wa ngano gramu 150

Maelekezo

Menya na katakata vitunguu, nyanya, pilipili na korosho. Pasha mafuta kiasi na kaanga vitunguu na nyama hadi ziive vizuri.

Ongeza vitu vilivyokatwakatwa, chumvi na pilipili. Pika hadi vimimina vyote vikauka kisha weka kando.

Chekecha unga na chumvi kwenye bakuli, ongeza mayai na maji ya kutosha kufanya unga mkorogo laini.

Weka kikaangio kilicho na mafuta kidogo juu ya moto wa wastani. Mimina unga kidogo kwenye sufuria na uueneze.

Kaanga mpaka uone kuna hudhurungi ya dhahabu pande zote mbili. Baada ya kumaliza, jaza pancakes na nyama halafu viringisha.

Pamba na nyanya, majani ya giligilani na upakue na mchuzi unaopenda.

 • Tags

You can share this post!

MAPISHI KIKWETU: Viazi vitamu vilivyookwa...

Wakili wa miaka 91 ashtakiwa kwa wizi wa Sh63.7 milioni  

T L