• Nairobi
  • Last Updated May 20th, 2024 6:55 PM
Wakulima wa miwa walia njaa viwanda vikisalia vimepigwa kufuli

Wakulima wa miwa walia njaa viwanda vikisalia vimepigwa kufuli

NA VICTOR RABALLA

WAKULIMA wa miwa kutoka magharibi mwa Kenya sasa wameitaka serikali kufungua tena viwanda vya sukari ili waweze kuuza mazao yao.

Wakulima hao waliibua wasiwasi kuwa kusitishwa kwa shughuli hizo kumewafanya wakulima wa miwa ambao wanategemea uzalishaji wa malighafi hiyo kushindwa kujikimu kimaisha.

“Kwa sasa, gharama ya maisha imepanda na wengi wameathiriwa wakiwemo wakulima wa miwa. Hii ndio maana tunaiomba serikali kufungua viwanda vya kusaga miwa,” akasema Saulo Busolo, mwenyekiti wa Muungano wa Kitaifa wa Mashirika ya Wakulima wa Miwa nchini (KNASFO).

Alilaumu serikali kwa kuchukua uamuzi wa kufunga viwanda bila kufanya mashauriano ya kutosha na wakulima wa miwa.

“Kufungwa kwa viwanda vya kusaga miwa kumewaacha wakulima wetu walio na miwa iliyokomaa kulemewa na gharama ya juu ya maisha.”

  • Tags

You can share this post!

El Nino: Wakazi wa South B wazibua mitaro ya majitaka

Fanyeni kazi au muende nyumbani, gavana wa Isiolo aonya

T L