• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 8:22 PM
Wamaua asikitishwa na tabia za wanaume kubaka watoto

Wamaua asikitishwa na tabia za wanaume kubaka watoto

NA MWANGI MUIRURI 

MBUNGE wa Maragua Bi Mary wa Maua amewataka wakuu wa kiusalama nchini kutangaza vita rasmi dhidi ya wanaobaka watoto.

Akizungumza katika eneo la Kambiti alikotembelea familia ya msichana wa miaka 7 anayedaiwa kubakwa na mwanamume wa familia, mbunge huyo alisema ushetani ulio na binadamu wengine unasikitisha.

“Badala ya kubaka watoto si uje hata kwangu? Ni unyama wa aina gani huu? Ni nini cha mtoto wa miaka saba kinaweza kuamsha hisia zako za mahaba? Anayekosa wa kumpa anachotaka aje kwangu nitampa hapa hadharani?” mbunge huyo wa chama cha UDA akafoka.

Wamaua alizitaka idara za kiusalama kumakinika zaidi na kuhakikisha wanaume wote walio na mawazo ya kishetani kubaka watoto wadogo wametupwa korokoroni na kuachwa kuozea humo.

“Mimi nikupate ukinajisi mtoto hata kabla polisi wafike haki ya mama nitakuwa…Acha nisiseme tu. Kuja kwangu useme shida yako ni hiyo tu na mimi niko na yangu. Nitakupa ikiwa hivyo ndivyo utaachana na watoto,” akasema.

Hisia za mbunge huyo ziliwafanya wenyeji kulia machozi ya huzuni huku wakishabikia utu wake katika kukemea udhalimu huo.

“Tunamuelewa mbunge wetu. Ameongea kama mzazi. Hizo ndizo hisia zetu pia. Tuwachane na watoto kabisa.

Wanaoelewa fasihi wanajua kwamba mbunge wetu hakumaanisha kwamba tuko tayari kuwahonga majambazi na yake bali alikuwa anawathubutu,” akasema Mzee wa Kijiji hicho.

Naibu Kamishna wa Murang’a Kusini, Bw Gitonga Murungi alisema yuko macho kujua wazee ambao huwa wanaandaa vikao vya kupatanisha wabakaji na familia za waathiriwa.

“Wazee kama hao hawana tofauti na wabakaji na nikawajua tu…Nyote mtajipata mahakamani kujibu mashtaka ya kushirikiana kunajisi,” akasema.

[email protected]

 

  • Tags

You can share this post!

William Kabogo akumbuka kanisa la alikozaliwa

Huddah Monroe: Ndoa si ndoto yangu, kwa nini nijipe...

T L