• Nairobi
  • Last Updated May 20th, 2024 9:16 PM
Wanaume wanaopenda pombe wanaandamwa na magonjwa 60

Wanaume wanaopenda pombe wanaandamwa na magonjwa 60

Na CECIL ODONGO

WANAUME wanaobugia pombe wanaandamwa na hatari ya kupatwa na aina 60 za magonjwa, utafiti umeonyesha.

Utafiti uliofanywa nchini China umefichua magonjwa mengine 33 ambayo yanaaminika kusababishwa na ubugiaji wa pombe.

Shirika la Afya Duniani (WHO), limekuwa likitambua magonjwa 28 yanayoaminika kusababishwa na pombe.

Miongoni mwa magonjwa yaliyothibitishwa na WHO ni ugonjwa wa ini, kiharusi (stroke) na kansa za tumbo kati ya mengineyo.

Lakini ripoti ya utafiti uliofanywa na wanasayansi wa Chuo Kikuu cha Peking (China) kwa ushirikiano na Chuo Kikuu Oxford (Uingereza), inaonyesha kuwa ugonjwa wa jongo (gout), macho (cataract), utepetevu wa mifupa na aina fulani za kansa kati ya maradhi mengineyo, pia yanasababishwa na ubugiaji wa mvinyo.

Ripoti ya hivi karibuni ya Mamlaka ya Kupambana na Dawa za Kulevya Nchini (Nacada) inaonyesha kuwa zaidi ya Wakenya milioni 3.2 – zaidi ya asilimia 70 wakiwa wanaume – wanabugia pombe kupita kiasi, hivyo kujitia katika hatari ya kukumbwa na maradhi hayo hatari.

Inakadiriwa kuwa asilimia 4 ya vifo nchini Kenya husababishwa na pombe, kwa mujibu wa WHO.

Asilimia 32 ya vifo hivyo hutokana na kansa na magonjwa ya akili yanayosababishwa na pombe.

Asilimia 19 ya wabugiaji wa pombe hufariki kutokana na maradhi ya moyo.

Ulevi pia umeshutumiwa katika kuongezeka kwa mizozo ya nyumbani na kuvunjika kwa familia.

 

 

 

  • Tags

You can share this post!

Waasi ODM walilia Ruto awaokoe

Muungano wa mapadri walia kulemewa na kiu cha mahaba

T L