• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 10:50 AM
Muungano wa mapadri walia kulemewa na kiu cha mahaba

Muungano wa mapadri walia kulemewa na kiu cha mahaba

NA MWANGI MUIRURI

MUUNGANO wa mapadri wa kiume ndani ya Kanisa la Katoliki wanaopinga imani ya kutooa wamesema wakati umefika wa kukubali ni vigumu kukaa bila jiko.

“Si unaona vile baadhi yetu tunakufa kwa lojing’i tukichovya asali? Wengine tumewekewa mchele kwenye vinywaji ndani ya mikahawa tukisaka uroda…Ili kuepuka hii hatari, acha tu tukubali ni vigumu kuishi na hisia za ngono ambazo hazitekelezwi,” akasema mshirikishi wa kampeni hizo Dikoni Edwin Wagura.

Bw Waiguru alisema kwamba “sio vyema kukaa katika mtazamo potovu wa kuumiza binadamu kwa itikadi ambazo hata hazieleweki ziliundiwa wapi”.

Akasema: “Tukizusha, wanatusomea injili ya Paulo aliyesema kwamba ikiwa unaona ugumu wa kukaa ukiwa mtakatifu bila ngono kama mimi wewe enda tu uoe”.

Bw Wagura alisema kwamba “Paulo sio wa kuaminika kwa kuwa mwanzo anakinzana na Mungu aliyesema katika maandiko matakatifu kwamba sio vyema mwanamume kuishi peke yake”.

Akaongeza: “Kabla Paulo aitwe hilo jina, alikuwa mwanajeshi aliyefahamika kama Saulo…Tabia za baadhi ya wanajeshi unazifahamu haswa wakati wameenda operesheni ambapo wanawake hulia wakidai kubakwa”.

Alisema kwamba huenda Paulo alikuwa amekula shibe yake ya mahaba enzi zake akiwa mwanajeshi, nguvu za kiume zikamwishia na ndiyo sababu alikuwa hashiriki ngono.

“Cha msingi ni kwamba, huu ukatili wa kuzima mwanamume aliye sawasawa kihisia uhuru wa kushiriki ngono unapaswa kuondolewa hata ikiwa ni kupitia maandamano au kesi mahakamani,” akasema.

Bw Wagura alisema, ni aibu mapadri kuaga dunia katika lojing’i na ndio maana wanapaswa kukubaliwa kuoa”.

 

[email protected]

 

  • Tags

You can share this post!

Wanaume wanaopenda pombe wanaandamwa na magonjwa 60

Wanawake wa kaunti waingie uongozini -Achani

T L