• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 10:50 AM
Wandayi: Dosari za KCPE huenda zikaibuka kwenye KCSE   

Wandayi: Dosari za KCPE huenda zikaibuka kwenye KCSE  

NA KASSIM ADINASI

KIONGOZI wa Wachache katika Bunge la Kitaifa, Bw Opiyo Wandayi amedai ubora wa matokeo ya Mtihani wa Kitaifa wa Kidato cha Nne (KCSE) utakuwa wa kutiliwa shaka sawa na KCPE ya mwaka huu, 2023.

Bw Wandayi Jumamosi, Desemba 9, 2023 aliwasuta Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu na mwenzake wa ICT Eliud Owalo kwa kufeli kupambana na magenge ya wahalifu waliovuruga matokeo ya KCPE.

“Ninahofia kuwa matokeo ya KCSE pia yatavurugwa sawa na yale ya KCPE. Machogu na maafisa wake walikosa kujibu maswali mengi na hii inaharibu elimu nchini,” mbunge huyo wa Ugunja akaeleza.

“Tunafahamu kwamba wizara za ICT na Elimu zinaendeshwa na watu ambao maadili yao ni ya kutiliwa shaka. Bw Machogu na Owalo hawana mamlaka yoyote kwani wizara zao zinaendeshwa na watu wengine,” Bw Wandayi akaongeza, bila kutoa ushahidi wowote.

Mbunge huyo wa upinzani alisema hayo kwenye kikao na wanahabari nyumbani kwake katika kijiji cha Madeya, eneobunge.

Lakini Waziri Owalo alikataa kushiriki mjadala huo kuhusu matokeo ya mitihani ya kitaifa ambayo yamevutia hisia kutoka kwa wadau mbalimbali.

“Siwezi kuzungumzia madai hayo wakati huu,” akasema.

Bw Wandayi alisema majibu ambayo Waziri Machofu alitoa kwa Kamati ya Bunge kuhusu Elimu kuhusiana na dosari zilizoibuka kwenye matokeo ya KCPE hayakuridhisha.

  • Tags

You can share this post!

Taulo za hedhi zilizotumika zazidi kuwa kero mitaa kadha...

Krismasi: Vijana wanavyopiga sherehe wakigeuza makazi yao...

T L