• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 3:46 PM
Krismasi: Vijana wanavyopiga sherehe wakigeuza makazi yao kuwa baa

Krismasi: Vijana wanavyopiga sherehe wakigeuza makazi yao kuwa baa

NA SAMMY WAWERU

MSIMU wa Krismasi unapobisha hodi kila mwaka, unajiri na shamra shamra za sherehe.

Krismasi, ni hafla ya kimataifa inayoadhimishwa Desemba 25 kila mwaka kwa minajili ya ukumbusho wa kuzaliwa kwa Yesu Kristu.

Siku hii maalum, hata hivyo, inaenziwa na kusherehekewa na Wakristu.

Na huku ulimwengu ukihesabu siku ili kuadhimisha Krismasi 2023, baadhi ya majengo ya kuishi hasa maeneo ya mijini yameanza kugeuzwa baa.

Aidha, washirika wanaandaa sherehe za kunywa pombe.

Wanalenga siku ya Ijumaa, wikendi; Jumamosi na Jumapili.

Wanatumia nyumba zao na zilizo wazi.

“Ploti za kukodisha baadhi ya wapangaji wamezigeuza kuwa baa. Wanaandaa mikutano ya kunywa pombe,” anadokeza Alfred Kimani, mmiliki wa ploti ya kupangisha Kasarani, Nairobi.

Kulingana na Kimani, majira ya usiku ploti zinazoathirika, wapangaji wasiotumia pombe wanahangaika kutokana na kelele za walevi.

“Hususan wenye watoto wachanga, wanapitia nyakati ngumu,” aelezea.

Inakuwa vigumu kuwapa notisi ya kuhama, baadhi wakiwa wamelipa kodi ya nyumba mwezi Desemba.

Joshua Omondi, keateka eneo la Ruiru, hata hivyo, anasema sherehe zinazohusiana na unywaji pombe zinaandaliwa na vijana.

“Wengi wao ni vijana. Badala ya kuenda kwenye baa au maeneo ya burudani, wananunua vileo na kugeuza nyumba zao kuwa majukwaa ya kunywa pombe,” akaambia Taifa Leo Dijitali kupitia mahojiano ya kipekee.

Isitoshe, wahusika ni wavulana na wasichana wachanga na wanapolemewa na makali ya pombe wanaishia kukosea wapangaji heshima.

“Nililazimika kuhamia Roysambu kutoka mtaa wa Githurai, kwa sababu ya tabia potovu nilizohofia zingeathiri watoto wangu wachanga kukua,” anasema Veronica Waweru, mkaazi Nairobi.

Cha kushangaza zaidi, baadhi wanajipata kushiriki ngono kiholela jambo linalozua hofu haswa kuwaweka kwenye hatari kuambukizana maradhi hatari ya Ukimwi na kushika mimba.

Kero hiyo inaathiri mitaa mingi katika Kaunti ya Nairobi.

Vituo vya kununua pombe kwa bei nafuu (wines and spirits) na ya kubeba, vimetajwa kuchangia hali kuwa mbaya zaidi.

Hata ingawa waraibu wa vileo wana haki kunywa, kisheria hawapaswi kuvuruga amani katika mazingira.

  • Tags

You can share this post!

Wandayi: Dosari za KCPE huenda zikaibuka kwenye KCSE  

MAKALA YA KIPEKEE: Kanisa linalohusishwa na kidosho...

T L